Muigizaji mkongwe aliyeigiza 'Independence Day na Homeland' James Rebhorn afariki dunia

Muigizaji mkongwe,James Rebhorn amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 65 na kwa mujibu wa agent wake Dianne Busch, muigizaji huyo amefariki kwa ugonjwa wa saratani ya ngozi (melanola).
Hollywood Reporter imeripoti kuwa muigizaji huyo amefariki nyumbani kwake New Jersey, Ijumaa asubuhi, March 21 na kwamba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka 1992.
Rebhorn aliyedumu kwenye tasnia ya filamu kwa miaka 50 alianza kufahamika zaidi baada ya kucheza kwenye filamu ya ‘Independece Day’ mwaka 1996, na alikuwa anaendelea kung’aa kwenye series ya ‘Homeland’ ambayo inaendelea kufanya vizuri hivi sasa ikiwa na simulizi la kigaidi na kipelelezi.
Previous
Next Post »