TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 24.03.2014
· MTOTO WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA AUAWA KWA
KUNYONGWA NA BABA YAKE MZAZI.
·
BIBI WA MIAKA KATI YA 60 - 70 AFARIKI DUNIA
BAADA YA NYUMBA ALIYOKUWA AKIISHI KUSHIKA MOTO.
·
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI CHEKECHEA ILONGO
AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
·
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KIWIRA AFARIKI
DUNIA BAADA YA KUSOMBWA NA MAJI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO MWENYE
UMRI WA MWAKA MMOJA NA MIEZI SABA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA HENRY JUMA MKAZI WA MIGOMBANI ALIKUTWA
AMEUAWA KWA KUNYONGWA SHINGO KISHA KULAZWA KITANDANI NA BABA YAKE MZAZI
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JUMA VENANCE.
TUKIO HILO LA
KUSIKITISHA LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014
MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO
KATIKA KATA YA MIGOMBANI, TARAFA YA TUNDUMA,
WILAYA YA MOMBA AMBAPO BAADA YA UHALIFU HUO, MTUHUMIWA ALIFUNGA MLANGO KWA NJE NA
KUFULI NA KUTOKOMEA MAHALI KUSIKOJULIKANA. WAPELELEZI PAMOJA NA RAIA
WALIPOVUNJA MLANGO NA KUINGIA NDANI WALIKUTA MAITI YA MTOTO HUYO IKIWA
KITANDANI. KATIKA CHUMBA HICHO WALIKUTA UJUMBE WA MANENO MENGI YALIYOANDIKWA NA
MTUHUMIWA, BAADHI YA MANENO HAYO NI “UNYAMA UNYAMANI, TUTAFUTE PESA KWANZA NIITE
J.M A.K.A GAIDI”. JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
BIBI MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LENNAR KALINGA,
MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 60-70
MKAZI WA IPINDA AFARIKI DUNIA BAADA YA NYUMBA YA NYASI ALIMOKUWA AKIISHI
KUSHIKA MOTO NA KUTEKETEA.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014
MAJIRA YA SAA 22:25 USIKU HUKO
KATIKA KATA YA IPINDA, TARAFA YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA. CHANZO CHA MOTO
HUO INADAIWA NI BAADA YA MAREHEMU AKIWA NA MUME WAKE KUWASHA KIBATARI KWA LENGO
LA KUFUKUZA SIAFU WALIOKUWA WAMEINGIA NDANI NA NDIPO MOTO ULIPO LIPUKA NA KUSHIKA
PAA LA NYUMBA HIYO LILILOKUWA LIMEEZEKWA KWA NYASI KAVU NA KUWAKA. MAREHEMU KWA
KUONA HIVYO ALIAMUA KURUDI NDANI YA NYUMBA HIYO KWA LENGO LA KUTOA VITU
VILIVYOKUWA NDANI NA NDIPO MOTO ULIPOMZIDIA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA KYELA.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUWA MAKINI NA MAJANGA YATOKANAYO NA MOTO KWANI YANA MADHARA MAKUBWA KWA JAMII.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWANAFUNZI WA
SHULE YA MSINGI CHEKECHEKEA ILONGO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ONESMO HAULE (6) MKAZI WA MKAZI WA
MAHENJE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJIRI T.597 BGU AINA YA TOYOTA
COASTER LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA STANLEY
ELIA MWANDA (44) MKAZI WA MWANJELWA JIJINI MBEYA.
AJALI
HIYO IMETOKEA MNAMO TAREHE 22.03.2014
MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOI CHA ILONGA, KIJIJI NA
KATA YA MAHENJE, TARAFA YA MLOWO, WILAYA YA MBOZI, MKOA WA MBEYA KATIKA
BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO KITUONI. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA VWAWA - MBOZI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA
SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI NA WALIMU KUWAELEKEZA WATOTO NAMNA SALAMA
YA KUVUKA BARABARA IKIWA NI PAMOJA NA KUVUKA KATIKA MAENEO YENYE VIVUKO [ZEBRA
CROSSING].
KATIKA TUKIO LA NNE:
MWANAFUNZI WA
SHULE YA MSINGI KIWIRA DARASA LA TATU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA EVA MATHIAS (11) MKAZI WA KIJIJI CHA
IBILIRO AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUSOMBWA NA MAJI YA MTO KIWIRA BAADA YA
KUTELEZA KATIKA DARAJA LILILOJENGWA KIENYEJI.
TUKIO HILO
LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.03.2014
MAJIRA YA SAA 09:00 ASUBUHI HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA ILONGO, KIJIJI CHA IBILIRO, KATA YA KIWIRA, TARAFA YA
UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE. WAKATI TUKIO HILO LINATOKEA MAREHEMU ALIKUWA NA DADA
YAKE AITWAYE VERO LUCAS (20) AMBAE ALITOA TAARIFA ZA KUTOKEA KWA TUKIO HILO
NA NDIPO JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZILIPOFANYIKA NA HATIMAE MWILI WAKE KUPATIKANA
MNAMO TAREHE 23.03.2014 MAJIRA YA
SAA 17:00 JIONI MAENEO YA CHUO CHA
MAGEREZA KIWIRA KATIKA MTO HUO HUO.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAZAZI/WALEZI KUACHA TABIA YA KUWATUMA WATOTO PEKE YAO MAENEO YA PORINI KWANI
NI HATARI HASA KIPINDI HIKI CHA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon