TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA
WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 22.03.2014.
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA MINNE AFARIKI
DUNIA AKIWA ANAOGELEA KATIKA MTO NZOVWE.
MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ALBERT LAZARO MWENYE UMRI WA MIAKA
MINNE, MKAZI WA ISONDA ITENDE AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUFA MAJI NA MWILI
WAKE UMEKUTWA UKIELEA KATIKA MTO NZOVWE ULIO JIRANI NA NYUMBA YAO.
TUKIO HILO LIMETOKEA TAREHE 21.03.2014 MAJIRA YA SAA
10:00 ASUBUHI HUKO MBALIZI, TARAFA YA USONGWE MBEYA VIJIJINI. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. UCHUNGUZI NA UPELELEZI
WA TUKIO HILO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI NA JAMII KWA UJUMLA KUWA MAKINI NA WATOTO WAO
IKIWA NI PAMOJA NA KUWAKATAZA KWENDA KUOGELEA AU KUCHEZA KARIBU NA MITO/MABWAWA/MADIBWI
YALIYOKO KARIBU NA MAENEO YAO KWANI NI HATARI HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA MVUA
ZINAZOENDELEA KUNYESHA. AIDHA ANATOA WITO KWA JAMII KUFUKIA/KUFUNIKA VISIMA NA
MADIBWI YALIYOKO KATIKA MAENEO YAO KWANI NI HATARI KWA WATOTO.
NYUMBA YENYE VYUMBA VIWILI YATEKETEA KWA MOTO JIJI
MBEYA.
NYUMBA MOJA YENYE VYUMBA VIWILI MALI YA FRANCIS SAMSON (31) MKAZI WA INYALA
JIJI MBEYA YATEKETEA KWA MOTO PAMOJA NA MALI ZOTE ZILIZOKUA NDANI YA NYUMBA
HIYO.
TUKIO HILO LA MOTO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 20.03.2014 MAJIRA YA SAA 12:45 MCHANA HUKO MTAA WA INYALA, KATA
NA TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA.
KATIKA TUKIO HILO MALI ZOTE ZILIZOKUWEMO NDANI YA
NYUMBA HIYO ZILITEKETEA KWA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA GODORO, KITANDA NA VYOMBO
MBALIMBALI AMBAVYO THAMANI YAKE BADO HAIJAFAHAMIKA.
CHANZO CHA MOTO HUO BADO HAKIJAFAHAMIKA. HAKUNA
MADHARA YA KIBINADAMU YALIYORIPOTIWA KUTOKEA. MOTO ULIZIMWA KWA JITIHADA ZA
WANANCHI, KIKOSI CHA ZIMA MOTO NA UOKOAJI PAMOJA NA JESHI LA POLISI. UCHUNGUZI
ZAIDI WA TUKIO HILO UNAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z.
MSANGI ANATOA WITO JAMII KUCHUKUA TAHADHARI NA MATUKIO YATOKANAYO NA MOTO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI:
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA
NDANDALO, KATA YA KYELA-KATI, TARAFA
YA UNYAKYUSA, WILAYA YA KYELA
TAREHE 21.03.2014 MAJIRA YA SAA 11:00 ASUBUHI MTU MMOJA
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SADICK JULIUS
(29) MKAZI WA KIJIJI CHA
NDANDALO ALIKAMATWA AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ILIYOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI AINA YA RIDDER KATONI MOJA [01].
MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA POMBE HIZO, TARATIBU ZA
KISHERIA ZINAENDELEA NA MARA ZITAKAPO KAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAFANYABIASHARA KUACHA MARA MOJA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UUZAJI NA
USAMBAZAJI WA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA PIA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO MWINGINE ULIOFANYIKA HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA YA
MAFYEKO,TARAFA YA KIPEMBAWE,
WILAYA YA CHUNYA TAREHE 20.03.2014 MAJIRA YA SAA 10:30 ASUBUHI MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA SAULO ZEPHANIA (48) MKAZI WA KIJIJI CHA
MAFYEKO ALIKAMATWA AKIWA AMELIMA/AMEPANDA ZAO HARAMU LA BHANGI MICHE 12 YENYE
UREFU FUTI 2.5 KWENYE SHAMBA LAKE LA
MAHINDI.
MTUHUMIWA NI MKULIMA WA ZAO HILO HARAMU, TARATIBU ZA KISHERIA ZINAENDELEA NA
MARA ZITAKAPO KAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA MARA MOJA KULIMA ZAO HARAMU LA BHANGI WALA KUUZA/KUSAMBAZA KWANI NI
KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI. AIDHA ANATOA WITO KWA
WANANCHI KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI ZA MTU/WATU WANAOJIHUSISHA NA
ULIMAJI/UUZAJI NA USAMBAZAJI WA BHANGI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[AHMED Z.
MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon