Msikilize Kaduguda akiwapa somo Simba, adai bado wapo watu wanaoweza kuiongoza


Audio: Kaduguda awapa somo Simba, adai bado wapo watu wanaoweza kuiongoza


Aliyekuwa katibu mkuu wa klabu ya Simba, Muhina Seif Kaduguda amewataka wanachama wa klabu hiyo, kufunguka kimawazo na kuamini bado kuna watu wenye uwezo wa kuongoza klabu hiyo kongwe nchini na ikafanikiwa kupata maendeleo kama zilivyo klabu nyingine duniani.
Kaduguda ametoa dongo hilo ikiwa ni baada ya mwenyekiti wa sasa wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage kutangaza dhamira yake ya kutowania tena nafasi ya uongozi klabuni hapo.
Kaduguda amesema tayari Simba ilikuwa imeanza kupata muelekeo wa kimaendeleo alipukuwa madarakani chini ya utawala wa Hassan Dalali, lakini bado mchango wake haukuthaminiwa na wanachama ambao waliamua kumuweka pembeni katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010.
Katika hatua nyingine Muhina Seif Mohamed Kaduguda amewataka wanachama wenzake wa klabu ya Simba kutorejea makosa ya kuchagua kiongozi kutokana na utajiri wake ama sifa aliyonayo katika jamii, na badala yake wajipange kumchagua kiongozi mwenye dhamira ya kuifikisha mbali klabu yao.
Uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba umepangwa kufanyika May 4 mwaka huu jijini Dar es salaam huku kamati itakayosimamia uchaguzi huo ikiteuliwa mwishoni mwa juma lililopita baada ya kamati ya utendaji kukutana.
Kamati hiyo ya uchaguzi wa klabu ya Simba inaongozwa na Mwenyekiti Damas Ndumbaro na Makamu wake, Salum Madenge pamoja na katibu Issa Batenga huku katibu msaidizi ni Khalid Kamguna.
Wajumbe ni Kassim Dewji, Juma Simba pamoja na Amin Bakhresa.
Msikilize hapa:
 CREDIT TO TIMES FM
Previous
Next Post »