MSAADA! KWA MSANII ISMAIL ISSA MAKOMBE (MAPEMBE) TUMA KWA TIGO PESA 0719985659/ 0784328963


Ismail Issa Makombe 'Mapembe' alivyo sasa.

MASKINI! Hali ya kiafya ya msanii wa Komedi Bongo, Ismail Issa Makombe ‘Mapembe’ inazidi kuwa mbaya kutokana na kuugua maradhi ya ini kwa muda mrefu huku ikidaiwa kuwa wasanii wenzake wamemtelekeza.

Mapembe ambaye anapiga mzigo katika Kampuni ya Al-Riyam inayozalisha kipindi cha vichekesho cha Vituko Show kinachorushwa kwenye Runinga ya Channel Ten, amelia  kuwa anateseka na ugonjwa huo tangu mwaka jana.

...Mapembe baada ya kuvimba tumbo.
Msanii huyo alifunguka kwamba alipimwa katika Hospitali ya Burhan, Dar na kuambiwa kuwa mwili wake umejaa sumu kwa asilimia 93 na ini limefeli huku akiwa ametokwa na vidonda usoni na tumbo lake kuvimba.
“Nimeamua kurudi nyumbani kwetu Mtwara ili angalau niombe msaada kwa ndugu na jamaa zangu niweze kuishi na kujaribu kupata matibabu zaidi.
...Wakati akiigiza.
“Hali yangu ni mbaya sana kwani mwanzo nilikuwa nikisaidiwa na bosi wangu ambaye naye kwa sasa anaonekana kuelemewa na majukumu yake, hivyo nawaomba sana wadau  waweze kunisaidia kwa sababu ninaumia sana.
“Imefikia hatua leo ninatambua kuwa wasanii wa filamu ni wanafiki, maana tangu mwaka jana hadi leo ninaumwa lakini hakuna hata mmoja aliyeweza kunisaidia zaidi ya Kitale ambaye alikuja kuniona,” alisema.
...Mapembe akiwa hoi.
Mapembe kabla hajaugua alikuwa akiigiza kwenye Kundi la Vituko Show  kwa kuvaa uhusika wa aina mbalimbali lakini mara nyingi alikuwa akifiti sana alipokuwa akiigiza kama askari wa usalama barabarani ‘trafiki’.
Yeyote aliyeguswa na matatizo ya msanii huyu anaweza kumsaidia kwa kutumia fedha kwa Tigo Pesa kwa namba 0719 985659 au Airtel Money kwa namba 0784 328963.
Previous
Next Post »