MAMBO MAKUBWA USIYOYAJUA ALIYOWAHI KUYAFANYA T.I.D


dfd
Top in Dar ndio maana halisi ya Jina lake hilo,ingawa kwa sasa ramani yake katika game hili,inazidi kufifia siku hadi siku na nafasi yake  kuwa Top hapa Bongo kushikiliwa na Diamond Platnumz.Ila kama ulikuwa hujui hii huyu ndiye aliyewahi kufanya maajabu katika industry hii ya Music wa Bongo Fleva.

King Crazy Gk ndiye msanii aliyemtambulisha rasmi kwenye hii sanaa ya bongo fleva na kufanya wapenzi  wa muziki wa Bongo fleva,watambue nafasi yake ya kipekee katika ramani ya Music,alishirikishwa kwenye Nyimbo ya GK ya Tutakukumbuka, kwa mara ya kwanza,TID akiwa amesimamia chorus ya nyimbo hiyo,hapo ndipo wadau wa music walipo gundua talent yake hiyo nakumpa dili la ku-record kwa kumgombania,hapo Poa Records.


Umaarufu wake ulianza baada tu ya kutoa single zake mwenyewe kwa mara ya kwanza ya, Mrembo na Zeze alizosuka Producer Pfunk chini ya Bongo records. Nyimbo yake yaZeze pekee iliweza kufanya viziri kiasi kwamba kuweza kupewa tuzo ya  Ijumaa Award for Best Song of 2002 na a Youth Action Award for Best Performing Artist of the Year,kwa kipaji chake matata cha kucheza,haikuwahi kutokea msanii aliyeweza kucheza kama TID,huku wasanii wengi waliofwata wakiwa wanaiga style za TID.
30578_389798013811_252408203811_3856240_1907505_n
Huyu ndiye msanii wa kwanza kuelezea story yake ya music kwa njia ya filamu,Girlfriendndio nyimbo aliyowahi kuitoa na kufanikiwa kuitengenezea movie,iliyoweza kumuweka kwenye ramani ya music East Africa na umaarufu Africa nzima,haijawahi kutokea hadi hivi sasa kwa mwanamuziki kufanya kitu kama hiki,cha kuweza kuielezea story ya nyimbo yake kupitia filamu.
girlfriend
Sauti ya Dhahabu,ikiwa ndiyo jina la album yake ya kwanza iliweza kuvunja record ya msanii yeyote yule kwa mauzo kwa wakati huo,baada ya kuuza zaidi ya copy 200,000 kwa Tanzania pekee,na zaidi ya copy 350,000 Africa .Hii ndio ilikuwa habari ya mjini,album iliyokuwa na ladha mchanganyiko wa muziki, ikiwa na mchanganyiko wa R&B na maadhi ya midundo ya Caribbean,huku single kama ‘Siamini’na ‘Kweli’zikiwa zinapewa airtime ya kutosha kila kona ya media hapa Bongo.
0886443553804_600
T.I.D hakuwa tu top in Dar,alikuwa ni top kwenye kila mioyo ya mashabiki wa muziiki wa Bongo fleva,kama ilivyo kwa msanii Diamond Platnumz hivi sasa,kuanzia kwenye nyimbo zake hadi kwenye style zake za uchezaji,huku kila mtoto aliyeweza kujaribu kucheza kama TID,alitaka ajulikane
Previous
Next Post »