Haya maaajabu eti Bibi wa miaka 92 ana mimba ya tangia mwaka 1948 mpaka leo soma hapa

NewsImages/823258.jpg

Bibi wa miaka 92 ambaye alipata mimba wakati wa ujana wake miaka 60 iliyopita anaingia leba kwaajili ya kujifungua mtoto huyo baada ya miaka yote hiyo kupita.

Huang Yijun hivi sasa akiwa na umri wa miaka 92 alienda hospitali baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo ndipo tatizo lake lilipowaacha madaktari midomo wazi.

Daktari aliyemfanyia uchunguzi bibi huyo alipigwa na butwaa baada kugundua kuwa bibi huyo mwenye umri wa miaka 92 alikuwa ana mimba.

Huang alizidi kumpagawisha daktari huyo baada ya kutoa maelezo ya mimba hiyo.

Huang alisema kuwa mwaka 1948 alipokuwa na ujauzito mtoto wake alifia tumboni. Baada ya kutakiwa atoe dola 150 na hospitali aliyopelekwa ili kukitoa kiumbe hicho tumboni, Huang alikataa kutoa kiasi hicho cha fedha na kuamua kurudi nyumbani kwake.

Kwa kupuuzia kutoa kiumbe hicho alichokuwa nacho tumboni Huang alinyamaza kimya bila kuwaambia ndugu zake kwa miaka yote hiyo.

Ukweli wa mambo umekuja kujulikana baada ya miaka 60 baada ya bibi huyo kuzidiwa na maumivu makali ya tumbo.

"Katika miaka yangu 40 ya udaktari wangu sijawahi kukutana na jambo kama hili, kiumbe kilicho tumboni inabidi kiondolewe haraka iwezekanavyo, kwa muda wote huo Huang kuwa hai pia ni muujiza mwingine"alisema daktari wa bibi huyo.



Previous
Next Post »