Baba aua mtoto kwa fimbo




WATU watatu wamefariki dunia katika matukio tofauti mkoani hapa likiwemo la mtoto Irene Mbembela (7), mkazi wa Sogea-Tunduma, wilayani Momba, kuuawa kwa kupigwa fimbo na baba yake mzazi.
Irene ambaye ni mwanafunzi wa chekechea katika Shule ya Msingi Migombani, alifariki dunia juzi, alfajiri alipokuwa akipatiwa matibabu katika kituo cha afya Tunduma.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, alimtaja mtuhumiwa kuwa ni Marco Mbembela mkazi wa Sogea, Tunduma wilayani Momba.
Alisema kuwa Mbembela alimpiga mwanae kwa kutumia fimbo sehemu mbalimbali mwilini ambapo alipoteza fahamu na kufariki dunia muda mfupi  alipokuwa akipokea matibabu hospitalini hapo
Previous
Next Post »