JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
RPC. Ofisi ya Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa
Mbeya,
Namba ya simu 2502572
S. L. P. 260,
Fax - +255252503734
MBEYA.
E-mail:- rp.cmbeya@tpf.go.tz
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 18.02.2014.
·
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA
WANANCHI HUKU MWINGINE AKIJERUHIWA MKOANI MBEYA.
·
MTU MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI
MBEYA AKIWA NA
BHANGI.
MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA WANANCHI HUKU MWINGINE
AKIJERUHIWA MKOANI MBEYA.
MNAMO TAREHE 17.02.2014 MAJIRA YA SAA
18:00HRS JIONI HUKO KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA JIJI NA MKOA WA MBEYA MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SELEMAN
KADUMU (25) MKAZI WA ILEMI ALIFARIKI DUNIA WAKATI ANAENDELEA KUPATIWA
MATIBABU HOSPITALINI HAPO. MAREHEMU PAMOJA NA MWENZAKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA DEVID SAMSON (26) MKAZI WA ILEMI
WALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA KUNDI LA WANANCHI
WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI HUKU WAKITUMIA SILAHA ZA JADI FIMBO NA
MAWE. CHANZO NI TUHUMA ZA WIZI BAADA YA MAREHEMU NA MWENZAKE HUYO MNAMO TAREHE 15.02.2014 MAJIRA YA SAA 23:45HRS USIKU KUVUNJA DUKA MALI YA
OMARY ABUU (20) MFANYABIASHARA NA
MKAZI ILEMI NA KUIBA REDIO AINA YA SUB – WOOFER, SIMU YA MKONONI NA COMPUTER.
MTUHUMIWA DEVID SAMSON ALIPATIWA
MATIBABU NA KURUDISHWA MAHABUSU. WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI
KWA MAHOJIANO ZAIDI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA
SHERIA NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
MTU MMOJA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA AKIWA NA
BHANGI.
MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA STEPHANO FESTO (25) MKAZI WA
SOGEA ALIKAMATWA AKIWA NA BHANGI KETE
TATU SAWA NA UZITO WA GRAM 15.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 17.02.2014 MAJIRA YA SAA
17:30HRS JIONI HUKO KATIKA MTAA WA SOGEA – TUNDUMA WILAYA YA MOMBA. KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA JAMII
KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon