WANAFUNZI SITA WANASHIKILIWA NA POLISI AKIWEMO NA MKUU WA CHUO MBARALI MBEYA

Na Saimeni Mgalula,Mbeya

Hali si swali kwa MKUU wa Wilaya ya Mbarali Gulamu Hussen Kiffu
kunusurika kuumizwa na wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Chimala
kilichopo Wilayani humo mkoani hapa baada ya kuvamia gari lake na
kuvunja vioo,kutoa upepo wa matairi  kutokana na Serikali kufunga chuo
hicho kwa kutokuwa na hadhi ya kudaili wanafunzi, watu watano
wamefikishwa mahakamani.

Kutokana na vurugu hizo zilizotokea chuoni hapo jana jioni, Jeshi  la
polisi Mkoani hapa linawashikilia wanafunzi  sita    akiwemo Mkuu wa
Chuo  hicho  Francis Mtega  kwa  tuhuma za kuhamasisha vurugu
zilizopelekea  kuharibu gari la Mkuu wa Wilaya ya  Mbarali.

Kamanda wa polisi Mkoani hapa Diwani Athuman  alisema  baada ya mkuu
wa wilaya kuongozana na baadhi ya viongozi wa serikali  hususani
kamati ya ulinzi na usalama wilaya kwa lengo la kutaka kujua sababu za
chuo hicho kuendelea kufundisha wakati serikali ilitoa agizo kifungwe
ndipo hapo walipovamiwa na wanachuo hao.

Alisema   tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya kuwasili Chuoni
hapo kwa  lengo la  kuzungumza na uongozi wa chuo ndipo baadhi ya
wanafunzi  walivamia gari la Mkuu wa Wilaya na kuanza kuvunja vioo kwa
kutumia mawena kisha kutoa upepo kwa malengo yasiyojulikana.

Kamanda Athumani alisema tukio hilo linaonesha ni mpango uliokuwa
umepangwa na uongozi wa Chuo  kwa muda mrefu kwani serikali ina
malengo mazuri kwa watanzania  na lengo kuu ilitaka chuo hicho
kisajiliwe  ili kitambulike  na Serikali na kuweza kutoa wauguzi walio
na sifa na kuwawezesha kupata ajira itakayotambulika serikalini.

Aliongeza kuwa  kitu cha kushangaza ni madaraka aliyonayo mkuu wa chuo
hicho ambapo yeye mwenyewe ni mwalimu na mhasibu na kwamba kulikuwa
hakuna sababu ya kufanya vurugu bali  kilikuwa ni kitu cha kutoa
vielelezo vya udaili wa chuo.

Alisema katika uchunguzi wa awali  umebaini kuwa chuo hicho kimeanza
muda mrefu na tayari  kimeweza kutoa wauguzi katika Nyanja mbalimbali
bila ya serikali kutambua  kama hakijasajiliwa na hakitambuliki.
Previous
Next Post »