Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma
ametangaza mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15
mwaka huu kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini.
Rais
Zuma ametangaza siku 5 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu
mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8,
2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi
nzima.
Tayari
msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia
nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinton na Waziri
Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha
kushiriki.
Sala
ya mazishi imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013
jijini Johanesburg.
Mwili
wake utawekwa katika jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia Desemba
11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa
mazishi,Rip Mandela.
EmoticonEmoticon