WILAYA YA MBARALI – MAUAJI.
MNAMO
TAREHE 13.12.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MPAKANI BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE KATA
YA IGAWA TARAFA YA RUJEWA
WILAYA YA MBARALI MKOA WA
MBEYA. MTU MMOJA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE,
JINSI YA KIUME MWENYE UMRI KATI YA MIAKA 37-40 ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUCHOMWA
KISU KICHWANI NA SHINGONI NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA
KANDO YA BARABARA HIYO. CHANZO CHA MAUAJI KINACHUNGUZWA. MWILI
WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA MBARALI KWA UCHUNGUZI. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA YA MAHALI ALIPO MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.
WILAYA YA MOMBA – AJALI
YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA
KIFO.
MNAMO
TAREHE 13.12.2013 MAJIRA YA SAA 14:30HRS HUKO MAENEO YA MTAA WA MWAKA
BARABARA YA TUNDUMA/SUMBAWANGA KATA YA TUNDUMA, TARAFA YA TUNDUMA, WILAYA
YA MOMBA, MKOA WA MBEYA. GARI T. 904 BXV AINA YA M/CANTER
LIKIENDESHWA NA DEREVA MAAMZEE S/O
MOHAMED, MIAKA 21, MNYIHA, MKAZI WA MTAA WA MWAKA – TUNDUMA LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU ASIYEFAHAMIKA
JINA WALA MAKAZI YAKE, JINSI YA KIKE,
UMRI KATI YA MIAKA 25-30 NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO CHA AJALI
NI MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA KWA
AJILI YA UCHUNGUZI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA NAIBU KAMISHNA WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA
MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA HASA KATIKA KIPINDI HIKI CHA
KUELEKEA MWISHO WA MWAKA.
Signed by:
[DIWANI ATHUMANI – DCP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon