Maandalizi ya mashindano ya
kombe la dunia yako hatarini kuingia dosari baada ya wafanyakazi wa viwanja
kadhaa ambavyo vinaendelea kujengwa kupanga kufanya mgomo .
Wafanyakazi hao wamepanga
kufanya mgomo baada ya kutoridhishwa na mazingira ya usalama kwenye maeneo ya
ujenzi .
Wafanyakazi hao wamekuwa
wakilalamikia hali ya usalama kuwa mdogo kwenye viwanja ambavyo ujenzi wake
haujakamilika baada ya kuwepo na matukio ya wafanyakazi kufariki dunia kwenye
maeneo ya kazi kutokana na ajali katika matukio tofauti .
Endapo mgomo huo utafanyika
maandalizi ya kombe la dunia yatakuwa yamepata pigo kutokana na baadhi ya
viwanja kushindwa kukamilisha ujenzi wake ndani ya muda uliopangwa.
EmoticonEmoticon