TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI“PRESS RELEASE” TAREHE 21. 11. 2013.




WILAYA YA  CHUNYA – AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
                                          KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 20.11.2013 MAJIRA YA  SAA 19:30HRS HUKO  KATIKA KIJIJI CHA MBUGANI,  KATA  YA  MBUGANI,   TARAFA YA  KIWANJA, BARABARA YA  CHUNYA/MBEYA  WILAYA YA  CHUNYA MKOA WA MBEYA, GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE  AINA YA  TOYOTA L/CRUISER  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU   OMARI S/O MWANGOSI,  MIAKA 75,  KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA KIJJI CHA MBUGANI  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE  PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. DEREVA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA  AJALI.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI  WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  AIDHA ANATOA RAIA KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.


WILAYA YA  MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.

MNAMO TAREHE  20.11.2013 MAJIRA YA  SAA 12:30HRS HUKO ENEO LA MWANJELWA, TARAFA YA  IYUNGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA JOSEPH S/O NGONYANI, MIAKA 22, MNGONI, MKULIMA, MKAZI WA SOKOMATOLA AKIWA NA NOTI MBILI ZA BANDIA @ TSHS 10,000/=, SAWA NA TSHS 20,000/=  ZENYE NAMBA BK-5487744. MBINU NI KUTAKA KUNUNUA BIDHAA KWA KUTUMIA NOTI HIZO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI MTUHUMIWA AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII /WAFANYABIASHARA KUWA MAKINI NA KIKUNDI/MTANDAO WA WATU WANAOJIPATIA PESA KWA MTINDO HUU KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA UNARUDISHA NYUMA MAENDELEO YAO NA KUWAHIMIZA WANA -MBEYA WALIOWEMA KUTOA TAARIFA ZA MAHALI WALIPO WATU/MTANDAO /KIKUNDI HICHO ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.


Signed by:
 [DIWANI ATHUMANI   - SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Previous
Next Post »