TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 19.11. 2013.





WILAYA YA  CHUNYA -  AJALI YA  PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU
                                           NA KUSABABISHA KIFO.


MNAMO TAREHE 17.11.2013 MAJIRA YA  SAA 18:00HRS HUKO  KATIKA KIJIJI CHA ISANGAWANA, KATA  YA  MATWIGA,   TARAFA YA  KIPEMBAWE,  WILAYA YA  CHUNYA  MKOA WA MBEYA, PIKIPIKI T.930 CNB AINA YA  SUNLG  IKIENDESHWA NA BESTON S/O MWALUGAJA,  MIAKA 30, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ISANGAWANA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO  KASSIM S/O ISMAIL  MIAKA 8,  MBENA, MKAZI WA KIJJI CHA ISANGAWANA  NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA  TUKIO.  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   MADEREVA KUWA MAKINI  WANAPOTUMIA VYOMBO VYA USAFIRI KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.  AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE,VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.


WILAYA YA  MBARALI – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 18.11.2013 MAJIRA YA  SAA 09:30HRS  HUKO KATIKA KIJIJI CHA CHIMALA  KATA YA CHIMALA  TARAFA YA  ILONGO  WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MSAFIRI S/O LAMECK, MIAKA 32, MSANGU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA MAPOGORO  AKIWA NA BHANGI YENYE UZITO WA KILO 29. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA SANDARUSI NA KUSUBIRI USAFIRI ILI KUISAFIRISHA KULETA MBEYA MJINI. MTUHUMIWA NI MVUTAJI NA MUUZAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KISHERIA  ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA   JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.



Signed by:
[DIWANI ATHUMANI- ACP]

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »