S/N
|
Tarehe
|
Muda
|
Maelezo
ya kosa/Tukio
|
Watuhumiwa
|
1.
|
20.10.2013
|
09:00hrs
|
MB/IR/9307/2013 – MAUAJI.
Huko
katika Kijiji cha Mjele, Kata ya
Mshewe, Tarafa ya Utengule – Usongwe
Wilaya ya Mbeya Vijijini Mkoa
wa Mbeya. FRANK S/O WILLIAM, miaka 30, Msafwa, mkulima na mkazi wa Mjele aliuawa
kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua
kujichukulia sheria mkononi wakitumia silaha za jadi fimbo na mawe. Chanzo
cha mauaji hayo ni tuhuma za wizi baada ya
marehemu kukutwa akiwa ameiba kuku watatu mali ya DISMAS
S/O RASHID. Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu
kwa mazishi. Upelelezi unaendelea kuwabaini na kuwakamata waliohusikana na
tukio hili.
|
----
|
2.
|
19.10.2013
|
20:30hrs
|
KYL/IR/2360/2013 –
MAUAJI.
Huko
katika Kijiji cha Lupembe, Kata ya Katumba Songwe, Tarafa ya Unyakyusa,
Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya. GODFREY S/O MWAKAPILA, miaka 21, Kyusa, mkulima na mkazi wa Kijiji
cha Mpunguti aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la
wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi wakitumia silaha za jadi fimbo
na mawe. Chanzo cha mauaji hayo ni tuhuma za wizi wa ng’ombe mmoja mali ya
MOTO S/O MWAKIANGE, miaka 36, Kyusa,
mkulima, mkazi wa Kijiji cha Muungano ambaye amekamatwa kwa mahojiano. Mwili wa marehemu umefanyiwa
uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi. Upelelezi unaendelea kuwabaini na
kuwakamata watu wengine waliohusikana na tukio hili.
|
01.
|
|
|
|
|
|
B:
Idadi ya watendaji.
Ø Jumla
ya askari 1,401 waliingia kazini,
doria na malindo mbalimbali.
Ø Jumla
ya watumishi raia waliopo ni 21.
Ø Jumla
ya vikundi vya ulinzi jirani ni 240, jumla ya
vikundi vilivyoshiriki ni 101 na walinzi 381 walishiriki
katika doria/malindo mbalimbali.
Ø Jumla
ya askari Mgambo waliopo ni 790
Ø Jumla
ya Polisi wasaidizi waliopo ni 420.
C:
Mafanikio yaliyopatikana.
§ Mafanikio
yaliyopatikana kupitia doria,misako na operesheni ni kama ifuatavyo:-
v Bhangi
– Nil
v Dawa
za kulevya {drugs} – Nil
v Pombe
ya Moshi -Nil
v Mirungi
– Nil
v Silaha
– Nil
v Nyara
za Serikali – Nil
D: Ukamataji wa makosa ya Usalama barabarani.
§ Jumla
ya makosa yaliyokamatwa – 91
§ Kesi
zilizopelekwa Mahakamani – Nil
§ Jumla
ya tozo [Notification] Tshs 2,430,000/=
E: Watuhumiwa waliokamatwa kwa
makosa mbalimbali.
- Jumla ya watuhumiwa waliokamatwa ni 18.
- Wahalifu wazoefu {Harbitual } – Hakuna.
- Wahalifu waangaliwa {Supervisee} – Hakuna
- Waliofungwa {Convicted}- Hakuna.
- Wahalifu waliachiliwa huru {Acquited}- Hakuna.
Nawasilisha tafadhali.
[P.A. MHAKO – ASP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA.
EmoticonEmoticon