TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 12. 10. 2013.






WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA     MIGUU NA
                                                 KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 11.10.2013 MAJIRA YA SAA 19:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA IYUNGA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE  LILIMGONGA  MTEMBEA KWA MIGUU  RAFIKI S/O MWASAKILA, MIAKA 83, KYUSA, MKAZI WA IYUNGA NA  KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO KINACHUNGUZWA. JITIHADA ZA KUMTAFUTA DEREVA AMBAYE ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA  ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.



WILAYA YA MBARALI – WIZI WA MIFUGO

MNAMO TAREHE 09.10.2013 MAJIRA YA  SAA 18:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISISI WILAYA YA  MBARALI MKOA WA MBEYA. SALUM S/O RAMADHANI, MIAKA 51, MKULIMA, MHEHE, MKAZI WA KIJIJI CHA ISISI ALIGUNDUA KUIBWA KWA NG’OMBE WAKE WATANO DUME WATATU NA JIKE WAWILI WENYE THAMANI YA  TSHS 1,500,000/= . MBINU NI WIZI MALISHONI. WATUHUMIWA WANNE WAMEKAMATWA WAKIWA NA NGOZI MOJA NA KICHWA KIMOJA CHA NG’OMBE AMBAO NI 1.NAVADI S/O MVINILE, MIAKA 42, MHEHE, 2. KANDAMBILI S/O CHESCO, MIAKA 28, MHEHE, MKULIMA 3. IBRAHIM S/O NYUMBARAGU, MIAKA 84, MKULIMA NA 4. HEMED S/O TARIMU, MIAKA 42, MHEHE, MKUKLIMA WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA ISISI – RUJEWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO  KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MAHALI WALIPO NG’OMBE WENGINE WALIOIBWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE ALIYEUZIWA/HIFADHI  MIFUGO  HIYO YA   WIZI AISALIMISHE MWENYEWE  MARA MOJA KATIKA MAMLAKA HUSIKA KABLA HAJATIWA NGUVUNI.
        


WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 11.10.2013 MAJIRA YA SAA 18:30HRS HUKO ENEO LA NZOVWE JIJI NA    MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA KELVIN S/O CHESAM, MIAKA 28, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA BHANGI KILO MBILI [02]. MBINU NI KUFICHA BHANGI KATIKA MFUKO MWEUSI WA RAMBO.  MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA MALI IDHANIWAYO KUWA YA WIZI.

MNAMO TAREHE 11.10.2013 MAJIRA YA SAA 06:00HRS HUKO ENEO LA SONGWE WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA    MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA HADASA D/O SENGO, MIAKA 20,  MNDALI, MKULIMA, MKAZI WA SONGWE AKIWA NA MIFUKO 57 YA  MBOLEA AINA YA  CAN NYUMBANI KWAKE MALI INAYODHANIWA KUWA YA  WIZI BAADA YA  KUSHINDWA KUITOLEA MAELEZO SAHIHI. MBINU NI KUFICHA MBOLEA HIYO NDANI YA NYUMBA.  TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO  KWA JAMII KUACHA TAMAA YA  KUJIPATIA KIPATO KWA NJIA ZISIZO SAHIHI KWA LENGO LA UTAJIRI WA HARAKA BADALA YAKE WATAFUTE MALI KWA NJIA HALALI.




 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Previous
Next Post »