|
WILAYA
YA MBEYA VIJIJINI - MAUAJI.
MNAMO TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA
16:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISUTO
– MLOWO WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. BOAZ
S/O SAMSON, MIAKA 25, MMALILA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA ISUTO ALIUAWA KWA KUCHOMWA KISU
TUMBONI NA BAKEL S/O MSAFIRI. CHANZO KINACHUNGUZWA, LAKINI UCHUNGUZI
WA AWALI UNAONYESHA NI KUDHULUMIANA
KATIKA MCHEZO WA KAMARI KATI YA MAREHEMU
NA MTUHUMIWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA ZAHANATI YA KIJIJI CHA ISUTO. MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA
TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANATOA WITO
KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA
MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA YA MOMBA – AJALI YA
GARI KUMGONGA MPANDA PIKIPIKI NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA 07:00HRS HUKO MPEMBA BARABARA YA TUNDUMA /MBEYA WILAYA YA MOMBA MKOA
WA MBEYA. GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA
LILIMGONGA MPANDA PIKIPIKI CERNANI S/O
SILUNGULE ,MIAKA 22, MNYAMWANGA, MKAZI WA MPEMBA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE
PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI WA
MWENDESHA GARI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. DEREVA
ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA
KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA
KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE
MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA NA GARI AZITOE ILI AKAMATWE NA
SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA
YA MBARALI - KUPATIKANA NA SILAHA.
MNAMO TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA 00:10HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIBETE – MKUNYWA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA SEBASTIAN S/O MARCUS,MIAKA 36, MHEHE, MKAZI
WA IGOMA WILAYA YA MUFINDI
MKOA WA IRINGA AKIWA NA SILAHA MOJA BUNDUKI AINA YA MARK
IV NO. BX- 10400 NA RISASI MBILI BILA KIBALI. MBINU NI KUFICHA SILAHA KATIKA MFUKO WA
SANDARUSI NA KUPAKIA KATIKA BAISKELI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI SILAHA BILA KIBALI KWANI
NI KINYUME CHA SHERIA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTU/WATU WANAOMILIKI SILAHA ISIVYO HALALI
AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
WILAYA
YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 16.09.2013 MAJIRA YA SAA 15:30HRS HUKO KATIKA ENEO LA META
JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI
WAKIWA DORIA WALIMKAMATA SAIMON S/O
MLOTWA,MIAKA 26, MSAFWA, MKAZI WA ILEMI
AKIWA NA BHANGI KETE SABA [07] SAWA
NA UZITO WA GRAM 35. MBINU NI KUFICHA
BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA SURUALI YAKE. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE
MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed
by:
[BARAKAEL N. MASAKI - ACP]
Kny: KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon