WILAYA YA CHUNYA – AJALI YA GARI KUPINDUKA NA KUSABAISHA KIFO NA
MAJERUHI.
MAJERUHI.
MNAMO TAREHE 04.09.2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAPOGORO BARABARA YA CHUNYA/MAPOGOLO
WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. GARI
T.198 AGT AINA YA M/FUSO LIKIENDESHWA NA DEREVA FRANSIS S/O MAHENGE, MIAKA 31, MKINGA,
MKAZI WA KIJIJI CHA KIBAONI LILIPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO CHA JOSHUA S/O MSUKULA, MIAKA 28, MLAMBYA,
MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA SINJILI NA MAJERUHI KWA WATU WATATU AMBAO NI 1.TUMAIN
D/OMAIKAMBO, MIAKA 30, KYUSA, MKULIMA MKAZI WA KIBAONI 2. ELIZA D/O BONIFACE, MIAKA 34, MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA SINJILILI
NA 3. JOSHUA S/O SHERIA, MIAKA 30,
MSAFWA, MKULIMA, MKAZI WA SINJILILI AMBAO WOTE WAMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA
CHUNYA. CHANZO KINACHUNGUZWA.
DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA
KULITELEKEZA GARI ENEO LA TUKIO. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE
KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE.
WILAYA
YA RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 04.09.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KIBUMBE – KIWIRA BARABARA YA
TUKUYU/MBEYA WILAYA YA RUNGWE
MKOA WA MBEYA. GARI T.993 AUL AINA YA SCANIA LIKIENDESHWA
NA DEREVA LUSUBILO S/O SEMI, MIAKA
33, KYUSA, MKAZI WA TUKUYU LILIMGONGA MPANDA BAISKELI AITWAE PHILMON
S/O EZEKIEL, MIAKA 22, MMALILA, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA KIBUMBE NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
DAKTARI WA SERIKALI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. CHANZO KINACHUNGUZWA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE
04.09.2013 MAJIRA YA SAA
11:45HRS HUKO ENEO LA MWANJELWA JIJI
NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA OSCAR S/O UZIWA, MIAKA 28,MZIGUA,MKULIMA,MKAZI WA MAJENGO AKIWA NA
KETE TISA [9] ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 45. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO WA SURUALI. MTUHUMIWA NI
MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA
KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA RUNGWE – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE
04.09.2013 MAJIRA YA SAA
19:30HRS HUKO MTAA WA MAGEREZA –
TUKUYU WILAYA YA RUNGWE
MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA
DORIA WALIMKAMATA LUSUBILO S/O JELAJELA,
MIAKA 35, KYUSA,MKULIMA,MKAZI WA MTAA WA MAGEREZA AKIWA NA KETE SITA [6] ZA BHANGI SAWA NA UZITO WA GRAM 30. .MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA
MVUTAJI WA BHANGI.TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA
WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA CHUNYA – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
MNAMO TAREHE
04.09.2013 MAJIRA YA SAA
16:15HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA KALOLENI
MKWAJUNI WILAYA YA
CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA
WALIMKAMATA EMANUEL S/O KISANGA,
MIAKA 25, MBUNGU,MKULIMA,MKAZI WA KALOLENI
AKIWA NA POMBE HARAMU YA
MOSHI[GONGO] UJAZO WA LITA SABA
[07]. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI
WA POMBE HIYO.TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO] KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA
AFYA YA MTUMIAJI.
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon