TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 21. 09. 2013.





WILAYA YA RUNGWE - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU 
                                                 NA KUSABABISHA KIFO.

MNAMO TAREHE 20.09.2013 MAJIRA YA SAA 12:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDAGA WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.565 AINA YA TOYOTA COASTER  LIKIENDESHWA NA  DEREVA SHABAN S/O IDDI, MIAKA 32, MKINGA, MKAZI WA TUKUYU  LILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO  KALEBO S/O EZEKIA,  MIAKA 5, KYUSA,  MKAZI WA KIJIJI CHA  NDAGA NA KUSABABISHA KIFO PAPO HAPO.  CHANZO MWENDO KASI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. DEREVA AMEKAMATWA, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYWA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. 




WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO]

MNAMO TAREHE 20.09.2013 MAJIRA YA SAA 15:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MBANGALA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA.  ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA PAUL S/O MAHAGA  MIAKA 22, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MBANGALA   AKIWA NA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA TATU [03]. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA  WITO KWA  JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA  MOSHI [GONGO]  KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.

Signed by:

                                                      [DIWANI ATHUMANI - ACP]
                                         KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »