WILAYA YA MBEYA MJINI -
AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA
06:30HRS HUKO MWANJELWA BARABARA
YA MBEYA/IRINGA JIJI NA MKOA WA MBEYA. GARI
T.387 BMN AINA YA TOYOTA COASTER
LIKIENDESHWA NA DEREVA HANSI S/O HUMPHREY, MIAKA 37, KYUSA,
MKAZI WA KYELA LILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU WESTON S/O HEPA MWALINGO,
MIAKA 83, MSAFWA, MKAZI WA AIRPORT NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI
ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA
MBEYA VIJIJINI - AJALI YA MPANDA
PIKIPIKI KUMGONA MTEMBEA KWA
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
|
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA
18:30HRS HUKO MBALIZI BARABARA YA
TUNDUMA /MBEYA WILAYA YA MBEYA
VIJIJINI MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI NA
DEREVA ASIYEFAHAMIKA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU REUBEN
S/O MWAKALOBO, MIAKA 22, KYUSA, MKULIMA, MKAZI WA MBALIZI NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE PAPO HAPO. CHANZO NI MWENDO
KASI . MTUHUMIWA ALIKIMBIA NA PIKIPIKI MARA BAADA YA TUKIO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI TEULE YA IFISI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI
KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA
NA PIKIPIKI AZITOE ILI AKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO
AJISALIMISHE MWENYEWE MARA MOJA.
WILAYA YA
KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA 20:00HRS HUKO KATIKA ENEO KYELA
KATI WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA LUGANO S/O RICHARD, MIAKA 23, KYUSA, MKULIMA,
MKAZI WA KYELA – KATI AKIWA NA BHANGI GRAM 20. MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KWENYE MFUKO
WA SURUALI YAKE. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI
HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA YA
MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO TAREHE 17.09.2013 MAJIRA YA SAA
10:00HRS HUKO KATIKA BAR IITWAYO NURU
INN ENEO LA MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI
MKOA WA MBEYA. ALIKAMATWA ERICK S/O JAMSON, MIAKA 25, MSAFWA,
MKAZI WA NZOVWE AKIWA NA NOTI BANDIA MOJA YA TSHS 10,000/= YENYE NAMBA – DT 2937833. MBINU NI
KUTAKA KUNUNUA VINYWAJI KWA KUTUMIA PESA HIYO. TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
JAMII HASA KATIKA MAENEO YA KIBIASHARA KUWA MAKINI NA MATUMIZI YA PESA ILI KUJIEPUSHA NA WATU WANAOTUMIA PESA
BANDIA . AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MTANDAO WA WATU WANAOMILIKI PESA BANDIA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI HATUA ZA
KISHERIA ZICHUKULIWE.
Signed
by:
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon