TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE” TAREHE 14. 09. 2013.




WILAYA YA  RUNGWE  – MHE.  DIWANI KATA YA  KIWIRA AKAMATWA KWA
                                           TUHUMA ZA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI.



§  MNAMO TAREHE 12.09.2013 MAJIRA YA  SAA 19:30HRS  HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KIBUMBE  KATA YA   KIWIRA – TUKUYU  WILAYA YA   RUNGWE MKOA WA MBEYA,  RAPHAEL S/O FRANK, MIAKA 42, KYUSA, MKULIMA NA MKE WAKE SUZANA W/O FRANK, MIAKA 38, KYUSA,  MKULIMA WOTE WAKAZI WA KIBUMBE KIWIRA – TUKUYU  WAKIWA NYUMBANI KWAO WALIGUNDUA KUTOWEKA KATIKA MAZINGIRA YA  KUTATANISHA KWA MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL, MIAKA 18, KYUSA, MWANAFUNZI KIDATO CHA NNE SHULE YA  SEKONDARI KIWIRA HIVYO JITIHADA ZA KUMTAFUTA ZILIANZA MARA MOJA  USIKU KUCHA BILA MAFANIKIO.

§   MNAMO TAREHE 13.09.2013 MAJIRA YA  SAA 06:00HRS WAZAZI HAO BAADA YA  KUONA MTOTO WAO HAKULALA NDANI KAMA ILIVYO KAWAIDA WALIAMUA KWENDA KATIKA KITUO CHA POLISI KIWIRA NA KUTOA TAARIFA YA  KUPOTELEWA  NA MTOTO.  HATA HIVYO MAJIRA YA  SAA 09:00HRS MTOTO WAO AGNES D/O RAPHAEL ALIRUDI NYUMBANI NA WAZAZI WAKE WALIPOMHOJI JUU YA  MAHALI ALIPOKUWA ALIWAJIBU KUWA   ALIKUWA NA MHE  DIWANI WA KATA YA  KIWIRA [CHADEMA]  LAURENT S/O MWAKALIBULE, MIAKA 28, KYUSA, MKAZI WA KIWIRA – KATI NA KWAMBA WALILALA KATIKA NYUMBA YA  MDOGO WAKE NA DIWANI HUYO AMBAYE JINA LAKE BADO KUFAHAMIKA NA KUWA KABLA YA  KUKUTANA WALIWASILIANA KWA NJIA YA  SIMU YA  KIGANJANI.

§  MTUHUMIWA AMEKAMATWA, UPELELEZI WA SHAURI HILI UNAENDELEA .


§  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA JAMII  HASA WANAFUNZI KUJIEPUSHA NA MADHARA YA  KUFANYA MAPENZI [NGONO] KWANI NI HATARI KWA  AFYA ZAO NA PIA KWA MAISHA YAO YA  BAADAE BADALA YAKE WAZINGATIE ZAIDI  MASOMO KWA FAIDA YAO , VIZAZI VYAO NA TAIFA KWA UJUMLA..




 [DIWANI ATHUMANI   - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »