“PRESS RELEASE”
TAREHE 08. 08. 2013.
WILAYA
YA RUNGWE – AJALI YA MPANDA PIKIPIKI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
|
MNAMO TAREHE
07.08.2013 MAJIRA YA SAA 17:00
HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA NDAGA WILAYA
YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. PIKIPIKI T.101 CDR AINA
YA T-BETTER IKIENDESHWA NA RASHID S/O
ISSA, MIAKA 32, MKINGA, MKULIMA MKAZI WA
KIJIJI CHA NTOKELA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO WILLY S/O EDWARD,MIAKA
5,MSAFWA MKAZI WA KIJIJI CHA NDAGA NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA
HOSPITALI YA WILAYA YA RUNGWE. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA
AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA
WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA
YA KYELA - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 07.08.2013 MAJIRA YA SAA 08:30 HRS HUKO KATIKA ENEO LA
KALUMBULU WILAYA YA KYELA
MKOA WA MBEYA. GARI T.932 BUF
AINA YA T/IPSUM IKIENDESHWA NA KAIMU S/O
HENDE, MIAKA 33, MBONDEI, MKULIMA MKAZI
WA KYELA-KATI ILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU MTOTO HAWA D/O GIBSON,MIAKA 6,MSAFWA,MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA S/MSINGI
MBUGANI MKAZI KALUMBULU NA KUSABABISHA
KIFO CHAKE PAPO HAPO. MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA
AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed
by:
[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon