Na Imelda Mtema WAZAZI ambao hawajajulikana
walikotokomea wamewatelekeza watoto wao wanne wanaoishi Kata ya Bangulo,
Pugu, Ilala, jijini Dar es Salaam, Amani lina mkasa wote. Mazigira
ya nyumba ya watoto hao ni ya kutoa machozi hata kwa mtu mwenye roho
ngumu kama jiwe. Nyumba iko hivyo, pa kulala ni chini, wadudu kibao huku
wakiwa hawajui hatima yao. Majirani ndiyo waliowaibua watoto hao
baada ya kubaini kuwa baba yao hajaonekana kwa miezi kadhaa nyumbani
hapo hali iliyosababisha wengine kulia. Akizungumza na paparazi wetu
juzikati, Sarah Shija (7) ambaye ndiye anayelea familia hiyo kwa sasa,
aliwataja wenzake, Kevin Shija (8), Babu Shija (5) na Brighton Shija
(6). Alisema mama yao mzazi aliondoka nyumbani hapo miaka miwili
iliyopita baada ya kutokea mzozo kati yake na baba yao na kwenda
kusikojulikana licha ya kwamba siku hiyo walimsihi sana mama huyo
asiondoke. Sarah aliendelea kuweka wazi kuwa, baada ya mama yao
kuingia mitini, baba yao ndiyo akawa kila kitu lakini kumbe na yeye
alikuwa na lake moyoni. Alisema miezi minne iliyopita, asubuhi baba
yao aliamka asubuhi na kuwaachia shilingi 5,000 na kiasi kidogo cha unga
kwenye kiroba na kuondoka akisema angerudi jioni. “Mara ya mwisho
baba alipoondoka alituambia angerudi jioni, akatuachia shilingi elfu
tano kwa ajili ya kununua mboga na vitu vingine,” alisema Sarah. Sarah alisema tangu siku hiyo baba yao hakurudi tena huku wao wakiwa wamebaki wenyewe na elfu tano aliyowaachia ikiwa imeisha. Alisema
hali hiyo iliwalazimisha kusimama masomo kutokana na ugumu wa maisha
kwa sababu mara nyingi wanaamka asubuhi wakiwa na njaa hivyo kushindwa
kuelewa kinachofundishwa na walimu. “Tunalala na njaa, tunaamka na
njaa, tunashinda na njaa sasa tusingeweza kwenda shule kwa sababu
tunakuwa tunatetemeka mwili. Hatujui baba atarudi lini,” alisema Sarah
na kuangua kilio. Alisema imefika hatua nduguze wakishikwa na kiu
anawapeleka kunywa maji machafu ya kwenye madimbwi ambayo pia yana
chumvi kupita kiasi kwa sababu hawana fedha (shilingi mia nne) ya
kununua maji salama. Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Sarah
alimuomba baba yao popote alipo kurudi nyumbani na kuendelea na maisha.
Pia walimtaka mama yao akisoma habari hii akawachukue kwani maisha yao
ni magumu sana na yeye analazimika kufanya shughuli nyingi za nyumbani
ili kuhakikisha uhai wao haukatishwi na njaa. Ili kujua maisha yao
zaidi ya kusikitisha usikose kuangalia Kipindi cha Wanawake Live cha
Mtangazaji Joyce Kiria ambacho kitaonesha ‘live’ maisha magumu ya watoto
hao.KUSAIDIA FAMILIA HII, TUMIA NAMBA HIZI:0754 021 501NA0713 612 533
EmoticonEmoticon