KLABU ya Chelsea iko katika hatua za
mwishoni za kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala
na dili hilo linaweza kukamilika ndani ya saa 48.
Tayari wamekwishamsajili Willian
kutoka Anzhi ambaye anasubiri kibali cha kufanya kazi leo na usajili wa
Eto'o utakuwa sehemu ya Pauni Milioni 32 zilizotengwa.
Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Cameroon utakuwa mfupi tu wa mwaka mmoja.
Eto'o alianzia soka yake Ulaya katika
klabu ya Real Madrid, lakini alicheza mechi tatu tu na akapelekwa kwa
mkopo katika miaka yake minne na klabu hiyo ya Jiji la Hispania.
Alitengeneza jina alipokuwa akichezea
Mallorca kabla ya kusajiliwa na Barcelona. Aliiwezesha kushinda Ligi ya
Mabingwa, akifunga dhidi ya Arsenal katika Fainali mwaka 2006.
Baadaye akaenda kuungana na Jose
Mourinho Inter Milan, na hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchaua kutua
Chelsea. Kocha huyo Mreno anaweza kuwa na imani naye zaidi kuliko
washambuliaji wake wa sasa, Fernando Torres, Romelu Lukaku au Demba Ba.
EmoticonEmoticon