Takribani
watu 54 wameuawa na wengine zaidi ya 3,000 wamejeruhiwa kufuatia
tetemeko kubwa la ardhi lililotokea katika eneo la milima la magharibi
mwa China.
Tetemeko
hilo lenye ukubwa wa 6.6 katika kipimo cha richta limepiga karibu na
mji wa Dingxi mkoa wa Gansu na kusababisha uharibifu mkubwa wa majumba
na kukata huduma za umeme.
Afisa mmoja wa eneo hilo amesema zaidi ya majumba 21,000 yameharibiwa vibaya na takribani 1,200 yameporomoka.
Mkoa
wa Ganzu, ambao ni eneo lenye milima, jangwa na malisho ya mifugo, una
jumla ya idadi ya watu milioni 26 ukiwa ni moja ya mikoa yenye watu
wengi zaidi nchini China.
Shirika
la Msalaba mwekundu la China limesema linapeleka katika eneo hilo
mahema, vifaa vya matumizi ya nyumbani pamoja na makoti ya baridi na pia
linayatuma makundi ya waokoaji kusaidia katika shughuli za kutoa msaada
kwa waathiriwa wa tetemeko hilo.
EmoticonEmoticon