“PRESS
RELEASE” TAREHE 09. 07. 2013.
WILAYA YA
CHUNYA - MAUAJI.
MNAMO TAREHE 08.07.2013 MAJIRA YA SAA
03:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MUHEZA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. GEDION
S/O PATSON LYENJE,MIAKA 36,MNYIHA,MKULIMA ,MKAZI WA KIJIJI CHA MUHEZA ALIUAWA
KWA KUKATWA SHOKA KICHWANI AKIWA NYUMBANI KWAKE . CHANZO NI WIVU WA KIMAPENZI
BAADA YA MAREHEMU KUGOMBANA NA MKE WAKE
AITWAE PRISCA D/O MSEMAKWELI,MIAKA 30,MNYIHA,MKULIMA MKAZI WA MUHEZA KUFUATIA
KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI KUTOKA KILABUNI KUNYWA POMBE . BAADA YA UGOMVI HUO MTUHUMIWA ALIKWENDA KILABUNI KUMCHUKUA HAWARA YAKE AMBAYE BADO
HAJAFAHAMIKA JINA NA KUJA KUMUUA MUME
WAKE . MTUHUMIWA PRISCA D/O MSEMAKWELI AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI
AFIKISHWE MAHAKAMANI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA KITABIBU
NA DAKTARI KISHA KUKABIDHIWA NDUGU KWA
MAZISHI .KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI
BADALA YAKE KUTATUA MATATIZO YA
KIFAMILIA KWA NJIA YA MEZA
YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MATATIZO
YANAYOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA MWINGINE ALIYEHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
WILAYA YA
MBEYA - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA
KUSABABISHA KIFO.
KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 08.07.2013 MAJIRA YA SAA 16:30HRS HUKO ENEO LA ITUHA JIJI NA MKOA WA
MBEYA. GARI T.192 BVC AINA YA TOYOTA
TERRADO LIKIENDESHWA NA DEREVA WILLE S/O TEMBA,MIAKA 30,MCHAGA, MKAZI WA
MAFIATI LILIMGONGA MTEMBEA KWA
MIGUU MTOTO DAVID S/O AMANI ,UMRI WA
MWAKA MMOJA NA MIEZI 7 ,KYUSA ,MKAZI WA ITUHA NA KUMSABABISHIA KIFO CHAKE PAPO HAPO . CHANZO NI MWENDO KASI . MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA NA GARI LIPO
KITUO CHA POLISI KATI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA
MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL MASAKI
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA
KUWA MAKINI WANAPOENDESHA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA
MOMBA
- KUPATIKANA NA MIRUNGI.
MNAMO TAREHE 07.07.2013 MAJIRA YA SAA
23:00HRS HUKO KATIKA NYUMBA YA KULALA
WAGENI IITWAYO MPAKANI ILIYOPO MTAA WA KILIMANJARO – TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA . ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MOHAMED
S/O MUSSA,MIAKA 27,MFANYABIASHARA MKAZI WA NAKONDE ZAMBIA AKIWA NA WENZAKE 12
WAKIWA WANATAFUNA MIRUNGI YENYE UZITO WA
KILO 1 GRAM 500. MBINU NI KUJIFUNGIA KATIKA MOJAWAPO YA VYUMBA VILIVYOPO NDANI
YA NYUMBA HIYO . TARATIBU ZINAFANYWA ILI
WAFIKISHWE MAHAKAMANI . KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA
ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA MOMBA - KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 08.07.2013 MAJIRA YA SAA 18:42HRS HUKO KATIKA KAMBI YA UJENZI WA BARABARA YA KICHINA IITWAYO CCC ILIYOPO KIJIJI CHA CHIPAKA - TUNDUMA WILAYA YA MOMBA MKOA WA MBEYA. ESSAU S/O KABUJE, MIAKA 56,MNDALI, MLINZI
MKAZI WA SIKANYIKA AKIWA KAZINI ALIMKAMATA
GODWIN S/O MUSHI,MIAKA 39,KAZI OPERATOR MKAZI WA MTAA WA MWAKA AKIWA NA BHANGI GRAM 250 . MBINU NI KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA MFUKO WA
RAMBO . MTUHUMIWA NI MVUTAJI WA BHANGI TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI BARAKAEL
MASAKI ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
WILAYA
YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA SILAHA [GOBOLE] .
MNAMO TAREHE 08.07.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO IVUMWE JIJI NA MKOA WA MBEYA.
ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA ZAWADI S/O ANDASON,MIAKA 27,FUNDI
UASHI, MKAZI WA ILOMBA AKIWA NA SILAHA MOJA AINA YA GOBOLE NYUMBANI KWAKE. KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA
KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUMILIKI
SILAHA BILA KIBALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.
Signed
By
[ BARAKAEL
MASAKI - ACP ]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon