TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI




 PRESS RELEASE” TAREHE 23. 07.2013.

WILAYA YA CHUNYA – MAUAJI

MNAMO TAREHE 21/07/2012 MAJIRA YA SAA 23:30HRS HUKO KIJIJI CHA NKWANGU WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA, SENI S/O SANDU, MIAKA 20, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA NKWANGU ALIUAWA KWA KUPIGWA FIMBO KICHWANI NA TOLO S/O SEKO, MIAKA 20, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA NKWANGU. CHANZO NI UGOMVI WA KUMGOMBANIA MSICHANA AITWAYE HOLO D/O KULWA, MIAKA 16, MSUKUMA MKULIMA NA MKAZI WA NKWANGU. MTUHUMIWA AMEKAMATWA NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAANDALIWA.  KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA KUDHIBITI HASIRA ZAO KWA KUYATATUA MATATIZO YA  KIMEPENZI KWA NJIA YA  MAZUNGUMZO ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUJITOKEZA.

WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 22/07/2013 MAJIRA YA SAA 17:00HRS. HUKO KIJIJI CHA MKWAJUNI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA REGNALD S/O ELIAS,MIAKA 33, MKULIMA, MNYAMWEZI NA MKAZI WA MKWAJUNI AKIWA NA BHANGI KETE 21 SAWA GRAMU 105. MBINU ILYOTUMIKA NI KUFICHA NYUMBANI KWAKE. MHUTUMIWA NI MTUMIAJI NA MUUZAJI WA BHANGI HIYO. TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA  KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


WILAYA YA KYELA – KUPATIKANA NA BHANGI

MNAMO TAREHE 22/07/2013 MAJIRA YA SAA 05:00HRS HUKO KIJIJI CHA IPINDA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA KATIKA MSAKO WALIMKAMATA JORAM S/O BROWN, MIAKA 25, MNYAKYUSA MKULMA NA MKAZI WA IPINDA AKIWA NA BHANGI MISOKOTO 4 PAMOJA NA FUNGUO ZA BANDIA 42. MTUHUMIWA NI MTUMIAJI WA BHANGI TARATIBU ZA KISHERIA ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA MARA MOJA  KUTUMIA DAWA ZA  KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.


Signed By,
 [DIWANI ATHUMANI – ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Previous
Next Post »