“PRESS RELEASE” TAREHE 11. 07. 2013.
WILAYA
YA MBARALI – MAUAJI
MNAMO TAREHE 10.07.2013 MAJIRA YA SAA
06:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA IPWANI WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. BANARIA
S/O NGELA, MIAKA 80, MHEHE, MKULIMA MKAZI WA IPWANI ALIKUTWA NYUMBANI
KWAKE AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA
KICHWANI NA SEHEMU MBALI MBALI ZA MWILI WAKE NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU
NI KUVUNJA MLANGO WA NYUMBA NA KUINGIA NDANI KISHA KUMUUA MAREHEMU AKIWA
AMELALA NDANI PEKE YAKE NA MKE WAKE MACHELINA D/O MSAGAMBE, MIAKA
70,MHEHE,MKULIMA, ALIKUWA AMELALA MSIBANI MTAA WA PILI . CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI
MAREHEMU ALIKUWA ANATUHUMIWA KUWA NI MCHAWI. MWILI WA MAREHEMU UMEFANYIWA UCHUNGUZI WA
KITABIBU NA DAKTARI KISHA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI
WA POLISI BARAKAEL MASAKI ANATOA WITO
KWA JAMII KUACHANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA IKIWA NI PAMOJA NA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI BADALA YAKE
KUTATUA MATATIZO YAO KUPITIA MEZA YA
MAZUNGUMZO NA KUWAFIKISHA KWENYE MAMLAKA HUSIKA WATUHUMIWA ILI KUEPUSHA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA JUU YA WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI WAZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.
WILAYA
YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI
MNAMO TAREHE 10.07.2013 MAJIRA YA SAA
07:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA UJERUMANI MAKONGOROSI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA MOSE
S/O DARD MIAKA 25, MGOGO MKULIMA MKAZI WA KIJIJII CHA UJERUMANI – MAKONGOROSI AKIWA
NA BHANGI YENYE UZITO WA KGM 1 . MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MVUTAJI WA BHANGI HIYO
TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAANDALIWA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI
BARAKAEL MASAKI ANAENDELEA KUTOA
WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Signed
By
[BARAKAEL MASAKI - ACP ]
KAIMU
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
EmoticonEmoticon