Nyota wa muziki Mariah Carey akimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa begaa lake l wakati akitengeneza video ya wimbo wake mpya.

Untitled

Nyota wa Muziki wa pop Mariah Carey ameteguka bega baada ya kubinuka wakati akitengeneza video nyimbo yake mpya.

Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alikuwa jijini New York akipiga picha za video za ‘remix’ ya nyimbo yake ‘Beutful’ akiwa na rapa machachari Young Jeezy wakati tukio hilo lilipo tokea.

Baadhi ya taarifa zinadai kuwa huenda muimbaji huyo aliteleza na kuanguka wakati akicheza katika video hiyo huku akiwa amevaa viatu vyenye kisigino kirefu (high heels), iliyokuwa ikiongozwa na mumewe Nick Cannon.

Carey alipelekwa hospitali ambako madaktari waliweza kurejesha vyema bega lakelililokuwa limechomoka mahali pake.

Wimbo wa ‘Beautful’ ambao Carey mwanzoni alirekodi na Mshindi wa tuzo ya Grammy na muimbaji wa RnB Miguel, ilishika namba 22 katika nyimbo moja moja huko Uingereza na kufikia namba 15 nchini Marekani.

Previous
Next Post »