Chama cha waziri mkuu nchini Zimbabwe kimesema
kuwa mmoja wa ofisa wake mkuu wa chama hicho amekamatwa baada ya
kuwasilisha ushahidi wa udanganyifu mbele ya tume ya uchaguzi nchini
humo.
Morgen Komichi aliifahamisha mamlaka baada ya
kugundua makaratasi ya kupiga kura yalikuwa yamewekwa katika kituo cha
kupiga kura mjini Harare ambapo maafisa wa jeshi walipiga kura za mapema
katika uchaguzi huo.
Alisema masanduku yote ya kura yaliyokuwa na kura za chama cha Movement For Democratic Change (MDC) yalitupwa.
MDC kinachoongozwa na waziri Mkuu Morgan
Tsvangirai, kimekuwa katika serikali ya umoja wa kitaifa na rais Robert
Mugabe wa ZANU PF , Umoja ambao umekuwa na mashaka ndani yake.
Uchaguzi nchini Zimbabwe umefanyika mapema Jumatano iliyopita.
EmoticonEmoticon