Gari la Kampuni ya Maziwa Tanga Fresh lanusurika kupinduka leo eneo la Ubungo mataa Jijini Dar.


SONY DSC
 Wakazi wa jiji la Dar es salaam wakikinga maziwa kwenye kontena la kampuni ya maziwa Tanga Fresh baada ya kichwa cha kontena hicho kuchomoka na kuacha njia eneo la Ubungo mataa   Julai 24, 2013.likitokea Mkoani Tanga hakuna aliejeruhiwa kwenye ajali hiyo.
SONY DSC
Ustaadh nae akijipatia maziwa bila kujali yana usalama au hapana.
SONY DSC
Jeshi la polisi likitawanya wananchi kwenye eneo la tukio.
SONY DSC
Kichwa chenye namba za usajili T 787 AFX lililobeba kontena la maziwa likiwa pembeni ya barabara mara baada ya kuacha njia likitokea Mkoani Tanga.
SONY DSC
Hapa asubuhi aaaah full chai ya maziwa na familia yangu…ndivyo anavyoonekana kijana huyo na ndoo yake mara baada ya kukinga lita za kutosha kutoka kwenye gari hilo.
SONY DSC
Umati wa wananchi ukiwa umekusanyika eneo la tukio kabla ya kutawanywa na askari wa jeshi la polisi
Previous
Next Post »