AFRIKA Kusini imesema afya ya Rais wa zamani wa nchi hiyo Nelson Mandela imeanza kuwa nzuri wakati jana amefikisha miaka 95.(HM)
Rais Jacob Zuma alituma salamu za pongezi za siku ya kuzaliwa kwa Mandela katika taarifa akisema kuwa Afrika Kusini inajivuna kumwona kiongozi huyo mashuhuri wa kimataifa ni wa kwao.
Mtoto wa kike wa Mandela Zindzi Mandela alithibitisha Alhamisi kwamba afya ya baba yake inaendelea kuwa nzuri.
Anasema kuna wakati hali yake ilikuwa mbaya na ya kutisha , lakini wiki tatu zilizopita ameonyesha mabadiliko makubwa .
Anasema ana uhakika baba yake atarejea nyumba hivi karibuni. Kiongozi huyo mtetezi dhidi ya ubaguzi wa rangi amekuwa katika hospitali mjini Pretoria kwa zaidi ya mwezi mmoja akisumbuliwa na maambukizo kwenye mapafu.
Mandela anasifika kote duniani kwa juhudi zake za kumaliza vita vya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Baadaye alichaguliwa kama rais wa kwanza mwafrika wa nchi hiyo mwaka 1994.
Chama cha kitaifa cha (ANC) kimesema kuwa katika siku hii ya kusherehekea siki ya kimataifa ya Mandela, ni heshima kwa miaka yake 95 kwa maisha yake aliyoishi vyema na ambayo ameitumia kupigania wananchi wa Afrika Kusini. Chanzo: bbcswahili na voaswahil
EmoticonEmoticon