Potiskum, Nigeria (AP) – Waislamu wenye siasa kali wamewaua wanafunzi 29 na mwalimu mmoja katika shambulio kwenye shule ya bweni Kaskazini-mashariki ya Nigeria.
Baadhi ya waathirika ambao bado wanatibiwa majeraha ya risasi na kuchomwa moto wamesema baadhi ya wanafunzi walichomwa moto wakiwa hai katika shambulio hilo kabla ya alfajiri ya Jumamosi (leo) katika shule ya sekondari ya serikali iliyopo mjini Mamudo jimboni Yobe.
Huku akitokwa na machozi ya uchungu pembeni ya miili ya wavulana wake wawili, mkulima Malam Abdullahi aliapa kuwaondoa wanae watatu waliobaki katika shule ya jirani.
Alilalamika kwamba kulikuwa hakuna ulinzi kwa ajili ya wanafunzi licha ya kupelekwa kwa maelfu ya askari tangu serikali ilipotangaza hali ya dharura katikati ya Mei katika majimbo matatu ya Kaskazini-mashariki.
Shule nyingi zimechomwa moto na idadi kubwa ya wanafunzi kuuawa wakiwamo zaidi ya waathirika 1,600 waliouawa na Waislamu hao wenye siasa kali tangu 2010.
EmoticonEmoticon