Mtangazaji wa Power Breakfast ya Clouds Fm Paul James a.k.a PJ afunga ndoa na Beatrice Wilbard Uiso.

 

IMG_2262

Maharusi Bwana na Bibi Paul James wakiwa na wapambe wao ndani ukumbi wa Shekinah Garden uliopo Mbezi Makonde wakisubiri kupokea zawadi kutoka kwa wageni waalikwa mara baada ya kumeremeta mwisho mwa Juma kwenye Kanisa la St. Gaspar Catholic la Kunduchi jijini Dar es Salaam.

IMG_2220

Bwana na Bibi Paul James katika pozi matata ndani ya ukimbi wa Shekinah Garden uliopo Mbezi Makonde mara baada ya kumeremeta katika kanisa la St. Gaspar Roman Catholic lililopo Kunduchi jijini Dar.

IMG_2224

Pichani juu na chini ni wageni waalikwa wakitoa mkono wa pongezi kwa maharusi.

IMG_2257
IMG_2146

Mrs. Paul James akiserebuka na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa mnuso wao wa nguvu uliokuwa ngumzo katika jijini la Dar es Salaam.

IMG_2386

MC wa Shughuli ambaye pia ni mtangazaji wa Clouds Fm Regina Mwalekwa akisherehesha.

IMG_2154

Picha juu na chini ni wageni waalikwa, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria harusi ya Bwana na Bibi Paul James mwishoni mwa juma ndani kiota chenye hewa safi cha Shekinah Garden kilichopo Mbezi Beach.

IMG_2156

IMG_2159

IMG_2168

Wadau wakibadilishana mawazo hapa na pale. 

IMG_2298

Mdau Isack Muyenjwa Gamba wa Radio One (kushoto) akiwa na baadhi ya wageni waalikwa huku wakitoa tabasamu bashasha mbele ya camera yetu.

IMG_2163

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akibadilishana mawazo na Mtangazaji wa Clouds Radio Gerald Hando wakati wa mnuso wa  Harusi ya PJ.

IMG_2209

Baba mzazi wa PJ akimkabidhi mwanae zawadi ya kimila Upinde na Ngao kama ishara ya kuilinda ndoa.

IMG_2213

Bwana harusi PJ akionyesha zawadi yake kwa wageni waalikwa.

IMG_2290

Kiongozi wa kikundi cha Umoja cha Kunduchi wakikabidhi zawadi yao kwa Maharusi.

IMG_2301

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akiongoza wafanyakazi wa kampuni yake kutoa mkono wa pongezi kwa maharusi. Kampuni ya Montage ilihusika kupendezesha ukumbi huu pamoja na kuandaa Cake ya Maharusi.

IMG_2307

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda na wafanyakazi wa kampuni yake wakitoa mkono wa pongezi kwa maharusi.

IMG_2327

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda akikabidhi zawadi ya Fungate (Honey Moon) kwa maharusi iliyotolewa na Serena Hotel kwa kushirkiana na kampuni yake.

IMG_2314 

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda na wafanyakazi wake katika picha ya pamoja na maharusi.

IMG_2331

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Montage Bi. Teddy Mapunda na wafanyakazi wake wakirudi kwenye siti zao.

IMG_2352

Wafanyakazi wa Clouds Media Group wakiongozwa na Sebastian Maganga (suti ya kijivu) kwenda kutoa mkono wa pongeza kwa mfanyakazi mwenzao.

IMG_2356

Clouds Media Group ikitoa mkono wa pongezi kwa maharusi.

IMG_2363

IMG_2378

Sebastian Maganga akitangaza zawadi kwa niaba ya Kampuni ya Clouds Media Group.

IMG_2384

Vicheko, nderemo na vifijo vilitawala ukumbini hapo..Kushoto ni MC wa Shughuli Regina Mwalekwa na Barbara Hassan (mwenye gauni jeusi) akiwa mwenye furaha kuona mtangazaji mwezie wa kipindi cha Power breakfast  kapata jiko.

IMG_2392

Power Breakfast ya Clouds Fm nayo haikubaki nyuma ilitoa voucher za Shopping kwa maharusi….. Mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast Gerald Hando akitangaza zawadi yao mfanyakazi mwenzao.

IMG_2433

Na hii ndio kamati ya maadalizi iliyofanikisha mnuso huo wa nguvu uliofanyika mwishoni mwa juma ndani ya Shekina Garden iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

IMG_2440

Maharusi Bwana na Bibi Paul James wakifungua muziki. Camera yetu iliishia hapo kama kuna picha za ziada basi tutawamuvuzishia.

IMG_2463

Kwenye Upande wa Video na Still Pictures ilihusika kampuni ya Ongea na Janet inayomilikiwa na Janet Sosthenes Mwenda ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Ongea na Janet. Pichani mwanadada huyo akiwa busy katika kuchanganya picha kwenye mnuso huo.

Previous
Next Post »