Baada ya kuwa katika
uchumba kwa muda mrefu hatimaye sasa Khamisi(H-Baba) na Khadija(Frola) wanafunga
ndoa,Jamaa anaefanya vizuri sana katika anga la muziki wa hapa nyumbani Tanzania
na Staili yake ya Bongo Bolingo H-Baba anatarajia kufunga zile pingu za maisha
na mwanadada ambaye anafanya vizuri katika tasnia ya filamu Bongo Movie Frola
mvungi ambye amesilim na kwa sasa anaitwa Bi Khadija.
Nilipata nafasi ya kuongea na H-Baba kuhusu ndoa yake hiyo wanayotarajia kufunga tarehe 8 ya mwezi wa 6, amesema kuwa harusi yao itakuwa ya kwaida sana kutoka na misingi ya kidini aliyokulia Khamisi, "eeh ndoa yangu mimi itakua ya kawaida sana kwasababu Masikini Anaoa, hakuna michango vaa jins vaa kanzu njoo, sisi hatuna mambo mengi wazazi wangu hawataki kabisa, mimi nimelelewa katika misingi ya kidini" Alisema H-baba.

EmoticonEmoticon