KIM NA KANYE WATANGAZA JINSIA YA MTOTO WAO ATAKAEZALIWA JULY


Kim Kardashian na Kanye West wanategemea kupata mtoto wa kike.Jinsia ya mtoto ilitangazwa wakati wa msimu mpya wa 8 wa reality show ya "Keeping Up With the Kardashians."

Camera ya kipindi hicho, ilimfata Kim hospitali alipokuwa na appointment na Dr wake, wakati yeye na dada zake Kourtney na Khloe, na mama yake Kris Jenner walijua jinsia ya mtoto huyo

Khloe alitangaza kwenye "Watch What Happens Live" kuwa Kim atajifungua mwezi wa 7. Kilichobaki midmoni mwa mashabiki wa Kanye na Kim ni kuhusu jina la mtoto, na jina la mtoto litaanza na herufi K???
siku ya jumapili marafiki wa Kim na familia yake walikutana kwa ajili ya baby showers ya Kim ambapo pia Kanye alihudhuria.




 
 
Previous
Next Post »