Freeman Mbowe na Godabless Lema wakiwa katika Uwanja wa Soweto jana mchana wakati zoezi la kuchukua vipimo mbalimbali likiendelea chini ya usimamizi wa wataalamu toka jeshini.

 
Mwenyekiti wa Chadema, Mh Freeman Mbowe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakiwa nyumbani kwa wazazi wa mmoja wa marehemu (Ramadhani) eneo la Mianzini kuwapa pole kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Dereva wa mgombea wa Chadema Kata ya Themi, Bwana Benny akiwa hospitali.
James Ole Millya na Mbunge Lema wakimjulia hali mmoja wa majeruhi walilazwa hospitali ya Seliani.
Eneo la maafa. Inaelezwa kuwa wataalamu wa jeshi waligundua kuwako kwa kitu ndani ya tanki la mafuta na hivyo kuamua kulikata. Taarifa hizo zinadai kwamba kulikuwa na mabomu yametegwa chini ya gari na hivyo tanki hilo lilishambuliwa kwa risasi labda utokee mlipuko! Pia gari hii ya matangazo lina majeraha mawili mlango wa kushoto yaliyotokana na kitu chenye ncha ambacho kinaweza kuwa risasi au vipande vya vyuma vya bomu.
Previous
Next Post »