WANAFUNZI WAANDAMANA USIKU WA MANANE, NI WALE WA SHULE YA WATOTO WENYE JIPAJI MAALUMU YA MZUMBE MORO.

 
Hii ndiyo kazi ya kuwazuia wanafunzi wenye vipaji wa shule ya sekondari Mzumbe iliyopo wilaya ya Mvomero baada ya wanafunzi hao kuandamana usiku wa manane kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Mor
ogoro, Joel Bendera ili kuweza kumweleza kero mbalimbali zilizpo katika shule hiyo hii ilikuwa Mei 29/ 2013. 
 
Mmoja wa wanafunzi akieleza jambo mbele ya viongozi waliofika kutafutia ufumbuzi wa kero hizo.
Gari la askari likiwa eneo la tukio wakati wakiwalinda wanafunzi hao huku wakimsubiri mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.
Askari wa jeshi la polisi akiwa katika lindo la kuwalinda wanafunzi hao.
Hapa wakipanda fuso kurudi shuleni baada ya mazungumza.
WANAFUNZI wa kidato cha kwanza hadi cha sita katika shule ya sekondari Mzumbe iliyopo wilaya ya Mvomero wamelazimika kuandamana kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wakishinikiza kuboreshewa huduma muhimu mkoani Morogoro.

Maboresha wanayodai kuboreshewa shuleni hapo ni pamoja na miundombinu ya vyoo, kuondoa ubadhirifu, uongozi mbovu na kukomeshwa vitendo vya lugha chafu zinazo tolewa na baadhi ya walimu.

Maandamano hayo yalizimwa na jeshi la polisi usiku wa manane (saa 8 usiku) baada ya jeshi hilo kupata taarifa za maandamano hayo na kulazimika kuwazuia katika eneo la Sangasanga barabara kuu ya Iringa-Morogoro wakati wakielekea kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera.

Wananfunzi hao ambao wana vipaji maalum wanadai kuwa maandamano hayo yanatokea baada ya kuvumilia kwa muda mrefu na hivyo wameamua kupaza sauti zao wakibainisha matatizo lukuki yanayo wasibu ambayo yanaweza kushusha kiwango cha taaluma yao.

Mkuu wa shule ya sekondari Mzumbe, Dismas Njawa ameelezea namna alivyoweza kutatua baadhi ya matatizo lakini hayakukidhi haja za wanafunzi hao.

Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Elia Ntandu alilazimika kwenda kuzungumza na wanafunzi hao asubuhi na kuahidi kuyafanyia kazi yale yatakayo wezekana.

Wanafunzi hawakuelewa, na ndipo Serikali ilipoamua kuifunga shule ya Sekondari ya vipaji maalumu, Mzumbe kwa muda usiofahamika na kuwapa wanafunzi siku mbili, kuanzia leo, kuondoka shuleni hapo.
Previous
Next Post »