MCHEZA MPIRA ADRIAN MUTU AOMBA KUMUASILI (ADOPT) MTOTO ALIEOKOLEWA BAADA YA KU-FALASHIWA CHOONI NA MZAZI WAKE

 

 

Mcheza mpira Adrian Mutu ameongea na Romanian channel PRO TV  kuhusu azma yake kutaka kumuasili (adopt) mtoto alieokolewa akiwa hai kutoka ndani ya bomba la kusafirishia maji taka ya chooni katika mji wa Jinhua, China mwanzoni mwa wiki hii.
mwanzoni mwa wiki hii, mtoto aliekuwa na uzito wa kilogram 2.268, kwasasa anajulikana kama baby 59 kutokana na kifaa alichokuwa amehifadhiwa, lugha ya kitaalamu kinaitwa "incubator", na kwa sasa yupo katika hali nzuri
Mutu,ambae kwa sasa anachezea Corsican side Ajaccio  amesema kuwa
"nimeshindwa kuelewa ni jinsi gani ningeweza kuendelea kuishi, kula chakula breakfast yangu, mara tu nilipoona habari hiyo kwenye TV. ni mtoto wa maajabu, nilipomuona huyo mtoto, nilisema, lazima nimuasili, ametuma kuja kwangu na Mungu,amenivutia sana huyu mtoto,nimemwambia mke wangu lazima tumsaidie, lazima tufanye kila tuwezavyo. sijawahi kufikiria kumuasili mtoto, sikuwa na plan yoyote kuhusu hili, lakini najua tu inabidi nimsaidie huyu."

licha ya kuwa na malengo haya chanya, mutu atakumbana na vikwazo kwasababu ni raia wa Roma na rai wa Roma hawezi kuasili mtoto kutoka China kwa sheria za sasa.

 


Previous
Next Post »