UCHAFU WAKITHIRI SOKO LA IKUTI JIJINI MBEYA










Wananchi wa Kata ya Iyunga mtaa wa IKuti  jijini mbeya wamelalamikia kitendo uongozi wa jiji la mbeya kushindwa kuzuia hali ya uchafu katika eneo la soko la Ikuti jijini

          Licha ya kuwepo kwa shughuli za kimaendeleo hasa soko na shughuli nyiingine hali imekuwa mbaya katika eneo la soko hilo kutokana na kuwepo kwa mirundikano ya uchafu katika ya soko hilo.

          Wakizungumza juu ya kuwepo kwa hali hiyo  wananchi wa maeneo hayo wamedai kuwa takataka zilizo jazana katika eneo hilo la soko linahatarisha afya za wakazi wa eneo hilo kutokana kuwepo na huduma muhimu kama soko ambako kunauzwa vyakula na mahitaji mengine.

        Mmoja wa wakazi hao ndugu  Janneth Mbukwa amesema kuwa kwa muda mrefu sasa takataka hizo zimekuwepo eneo hilo licha ya wafanyabiashara wa eneo hilo pamoja na baadhi ya wananchi kutoa taarifa sehemu husika ili kulifanyia kazi suala hilo.

        Amesema kuwa licha ya kuwepo kwa uchafu huo  kwa muda mrefu bado mawakala wa kutoza ushuru wamekuwa wakikusanya michango kama kawaida    Licha ya kuwepo kwa hali hiyo ambayo ni adha kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.

        Amesema tatizo kubwa lililopo katika eneo hilo ni harufu mbaya inayo toka eneo hilo ambapo kwa asilimia kubwa huathiri shughuli  zilizopo katika eneo hilo ambapo zaidi ya vibanda 20 vya mama ntilie  vipo eneo hilo la ghuba la taka hali ambayo imefanya wateja wao kuwa na hofu juu  ya afya zao.


Previous
Next Post »