Hili ndo kanisa la olasiti....Mlipuko ulipotokea mapema asubuhi
Hii ni sehemu ambayo mlipuko umetokea asubuhi katika kanisa la olasiti hapa arusha
Mt.meru hospital....Ndugu na jamaa wakiwa nje ya hospitali kusubili taarifa za waliojeruiwa katika mlipuko uliotokea mapema asubuhi kanisani olasiti Umati wa wananchi wa mkoa wa Arusha wakiwa njiani kuelekea kuangalia ndugu na jamaa zao waliokuwamo kwenye ibada hiyo inasadikika majeruhi zaidi ya thelathini na watano wapo hospitali huku kukiwa hakuna taarifa ya vifo. Kanisa lililolipuliwa likiwa linaonekana kwa mbali huku wananch wakilitazama kwa mbali kutokana na tishio la kutokea kwa milipuko mingine ...Mtu mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hilio wakati wengine wanasadikika kukimbia. Waumini pamoja na baadhi ya wanacchi wakiwa katika hali ya taharuki wasiamini nini kilichotokea kutokana na mlipuko mkubwa uliotokea asubuhi ya leo.
Polisi wakijaribu kuchunguza eneo bomu lilipolipukia leo asubuhi wakati wa misa ya kuzindua kigango hicho.iliyo katika kata ya olasiti na parokia ya burka. Polisi waki imarisha doria eneo la tukio baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali kupatiwa matibabu zaidi ...Mpaka tunaondoka eneo la tukio Viongozi mbali mbali akiwemo mmbunge wa arusha walikuwemo eneo hilo.
Majeruhi wa tukio hilo wakiwa katika hali mbaya..
EmoticonEmoticon