NAMNA MONIQUE ALIVYOPUNGUA UZITO!


 
Kwa miaka mingi nimekuwa shabiki wa Monique, Monique Angela Hicks msanii wa filamu na comedy wa Marekani.Baadae nikaanza kumfatilia na talk show yake ya the Mo'Nique show ambayo sikuipenda hakunifurahisha kwa kweli.Nampenda kama muigizaji na comedian baasi.
Kwa miaka yote namfatilia kama mwanamke mnene kweli kweli ikawa kama identity yake.Toka kwenye vichekesho vya the parkers kwa wale mnaovikumbuka alikuwa kibonge.
 Amecheza movies kibao niipendayo zaidi hizi ya Phat girls,Welcome Home Roscoe Jenkins,Two Can Play That Game,Precious filamu iliyompa tuzo nyingi sana mwaka 2009 na zingine kibao.
 Monique akiwa na mumewe Sidney Hicks ambae wamefahamiana toka wadogo wakiwa na miaka 14.Kabla alikuwa ameolewa alipoachika ndio akaoana na Hicks.Ndoa ambayo wao wanaiita open marriage 'hakuna siri'
Ikitokea umeona mtu mmetamaniana hakuna siri hata kama mmefaya tendo ukweli mezani maisha yanaendelea.Hakuna kuachana kisa mmoja ametembea na mtu nje ya ndoa duhhh!

Kwa muda sijamuona kwenye movies au popote hata talk show yake ilisimamishwa BET.Na mara ya mwisho kumuona alikuwa kapungua kiasi kutoka ule unene wake wa zamani.


Majuzi zimetoka picha zake akiwa kapungua sanaa hata ningeulizwa ni nani nisingemtambua.Sijui kwa nini nilikuwa nampenda alipopungua kidogo tu.Siri yake kubwa ni kula vizuri kwa afya na mazoezi ya nguvu.
Previous
Next Post »