BAADA ya kukwepa shitaka la ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare, leo ana anza mtihani mwingine wa kutafuta dhamana.
Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kumfutia Lwakatare mashta ya ugaidi yaliyokuwa yakimkabili yeye na mwenzake Joseph Ludovick Rwezaura, ambayo haikuwa na dhamana , hivi sasa wanashtaka moja la kula njama ambalo linadhaminika.
Kesi hiyo namba 6 ya mwaka 2013, inayosikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, inatajwa leo, lakini mawakili wa Lwakatare wamejipanga kumwombea dhamana Lwakatare.
Akizungumza na Habarimpya.com mmoja wa mawakili wa Lwakatare, Peter Kibatala alisema kuwa kosa lililobaki linadhaminika, hivyo jambo moja watakachokifanya leo ni kuwasilisha maombi ya dhamana tu.
“Kwa kuwa shtaka lililobaki linadhaminika, na kwa kuwa tayari file ( jalada) la kesi limeshwarejeshwa (Kisutu) kutoka Mahakama Kuu, basi tutakachokifanya leo (kesho) ni kuomba dhamana tu” alisema Wakili Kibatala na kuongeza:
“Kama hapatakuwa na pingamizi lolote tunaamini kuwa leo anaweza kutoka kwani tumejiandaa kutekeleza masharti yoyote yatakayotolewa na mahakama.”Ikiwa hapatakuwa na pingamizi lolote la kisheria kutoka upande wa mashataka ambalo litaibua mabishano makali, huwenda mahakama ikatoa uamuzi wa maombi ya dhamana leoleo na kama wataweza kutimiza masharti yatakayowekwa na mahakama, basi Lwakatare anaweza kurejea uraiani leo.
Hata hivyo kama kutakuwa na pingamizi la kisheria na mabishano mahakama inaweza kuahirisha na kupanga siku nyingine ya kutoa uamuzi wa maombi hayo ili kupata muda wa kutafakari kwa kina hoja za kisheria za pande zote zitakazokuwa zimetolewa. Lwakatare na Rwezaura walikuwa wakikabiliwa na mashtaka manne, matatu kati yake yakiwa ya ugaidi na moja la kawaida la jinai. Mashtaka hayo yalikuwa ni kula njama, kupanga kumteka Dennis Msacky na kisha kumdhuru kwa kutumia sumu, na kufanya mkutano wa vitendo vya kigaidi.
Mashtaka hayo matatu yalikuwa yakiwakabili washtakiwa wote wawili wakati shtaka la nne la kuhamasisha vitendo vya ugaidi lilikuwa likimkabili Lwakatare peke yake, akidaiwa kuruhusu nyumba yake ya Kimara King’ongo kutumika kupanga mipango ya ugaidi. Hata hivyo
EmoticonEmoticon