Kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson atangaza kujiuzulu kufundisha timu hiyo

 

 

KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ametangaza kustaafu kufundisha soka ikiwa ni miaka 27 tangu aanze kuifundisha timu hiyo mwaka 1986.

Ferguson anaondoka United akiwa amebeba mataji 30 huku pambano la mwisho la msimu huu dhidi ya West Brom likiwa la 1,500 tangu aanze kuifundisha Manchester United.

Bado haijajulikana ni kocha gani atarithi mikoba ya Ferguson ingawa inatajwa kuwa kocha David Moyes wa Everton anapigiwa chapuo la kuwa kocha mpya wa timu hiyo.

Previous
Next Post »