Katika kuadhimisha Siku ya Ulaya Mei 9 Umoja wa Ulaya kufanya mkutano maalum na Wizara ya Fedha.

 

Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Filiberto Cerian-Sebregondi (wa tatu kulia) kwa pamoja na wakuu wa Idara za nchi Wanachama wa Umoja huo jana wamefanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuzungumzia maadhimisho ya Siku ya Umoja wa  Ulaya yanayotarajiwa kufanyika tarehe 9 mwezi huu.

Balozi Filiberto Cerian-Sebregondi amesema katika kuzindua wiki ya Umoja wa Ulaya 2013 jijini Dar es Salaam na Arusha kutazinduliwa shughuli mbalimbali ikiwemo mafunzo juu ya haki za binadamu yatakayotolewa kwa waandishi wa habari na wahariri 70 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania yatakayoandaliwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Ameongeza kuwa siku hiyo hiyo Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Concern Worldwide (Tanzania) watazindua Mradi wa haki za Kijamii na Kiuchumi kwa Wanawake.

Balozi huyo amesema maadhidimisho ya Wiki ya Ulaya 2013 yataanza Mei 7 2013 hadi siku ya kilele Mei 9 na kuendelea hadi Mei 12 2013.

Aidha ametumia fursa hiyo kwa niaba ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kutoa pole kwa rais na watanzania kwa ujumla kutokana na tukio la jumapili la mlipuko unaodhaniwa kuwa ni bomu kutokea kanisani mkoani Arusha wakati waumini wajiandaa kwa ibada. Wengine ni Balozi wa nchi mbalimbali wa Jumuia ya Umoja wa Ulaya.

Sehemu ya waandishi wa habari na viongozi wa taasisi mbalimbali zinazofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.

Previous
Next Post »