Operation Manager wa Mo Blog Zainul Mzige akiwa nje nyumba ya ambayo ndiyo makazi ya Askofu Mkuu Desmond Tutu iliyopo Soweto nchini Afrika Kusini ambapo waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali barani Afrika walipata fursa kutembelea makazi hayo wakati wakipokwenda kushuhudia uzinduzi wa shindano la Big Brother The Chase lililozinduliwa Jumapili iliyopita ambapo ziara ya waandishi hao ilidhaminiwa na Kampuni ya Multichoice Africa. (Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
Pichani juu na chini ni waandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali barani Afrika wakipiga picha za ukumbusho nje ya nyumba ya Askofu Desmond Tutu mwanaharakati maarufu wa kutetea Haki za Binadamu.
Pichani juu na chini ni muonekano wa nje wa makazi ya Askofu Tutu ambapo kwa sasa inaishi familia yake.
Barabara inayoelekea yalipo makazi ya Askofu Desmond Tutu.
Wenzetu Bwana wameendelea kwelikweli kila mtaa na barabara una kibao kinachotoa maelekezo ya mahali unapokwenda, Chezea Bongo Wewe taa zetu barabarani kila siku zinagongwa na magari na vibao vya maelekezo ya mtaa ndio hadithi mpya manake Hakunaga……
Hii ni Nyumba ya mtetea haki za Binadamu maarufu Askofu Desmond Tutu wa Afrika Kusini ambaye amewahi kushinda tuzo ya Amani mwaka 1984 kwa kuongoza harakati za kupinga ubaguzi wa rangi bila vita .
Alithibitishwa na aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Haki na Maridhiano .
Hapa pamekuwa nyumbani kwa Askofu Desmond na mama Leah Tutu tangu mwaka 1975 .
Wamesherehekea maadhimisho ya miaka 50 ya ndoa katika nyumba hii ambayo bado ni makazi yao katika jiji la Johannesburg.
Kwa kuongezea tu nyumba hii ilibuniwa na Mhandisi Jo Noero mnamo mwaka 1990.
Nyumba hii imezinduliwa Oktoba 15 mwaka 2011.
Idadi ya watu wa Afrika Kusini ni takriban milioni 52 ambapo kati yao milioni 42 ni Weusi, milioni 5 ni weupe kwa maana ya wazungu na milioni 5 ni mchanganyiko na waasia milioni mbili 2 ambao wengi wao ni wahindi na Wachina.
EmoticonEmoticon