Pichani: Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi (katikati) akiwa pamoja na Katibu wake, Mchungaji Palemo Massawe (kulia) na Ofisa Habari wa Taasisi hiyo, Sailas Malula wakionesha mfano wa hundi ya Shilingi Milioni moja ambayo wanataraji kuikadhi Hazina kwaajili ya kununua ndege mpya ya serikali. Taasisi hiyo ambayo inajishughulisha na maombi imewaambia wana habari kuwa imeamua kuendesha zoezi hilo kwaajili ya kununua ndege mpya ya Rais.
Mwenyekiti wa Good News for All Ministry, Askofu Charles Gadi (kulia) akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam jana juu ya kuendesha zoezi la kuchangisha fedha zitakazotumika kununulia ndege mpya ya Rais. Kushoto kwake ni afisa Habari wa Taasisi hiyo Ndg. Sailas Malula.
EmoticonEmoticon