ARIEL CASTRO AFIKISWA MAHAKAMANI OHIO


Ariel Castro aliyeteka nyara wasichana watatu kwa miaka 10, Cleveland, Ohio May 9, 2013 Ariel Castro aliyeteka nyara wasichana watatu kwa miaka 10, Cleveland, Ohio May 9, 2013.

KESI ya utekaji nyara wa wasichana watatu wa Marekani yashtua wengi Marekani na nje ya Marekani.
Dereva wa zamani wa basi la shule kutoka jimbo la Ohio, Marekani Ariel Castro anayeshutumiwa kuwashikilia mateka wanawake watatu katika nyumba yake kwa mwongo mmoja, alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Alhamisi akiwa ameinamisha kichwa chake chini wakati jaji akiwa ameweka dhamana kubwa katika kesi yake. Castro hakusema lolote wakati  wa kusomewa  mashataka.

Jaji wa Cleveland katika jimbo la Ohio aliamuru kuachiwa kwake  kwa dhamana ya dola milioni nane , kiasi ambacho Castro ambaye hana ajira hawezi kum
udu na hivyo kubaki jela mpaka  kesi yake itakaposikilizwa tena.

Mwendesha mashtaka alisema Castro aliwanyanyasa kingono wanawake aliowateka kati ya mwaka 2002 hadi 2004 na kuwaweka katika nyumba yake kwa mwongo mmoja. Mwendesha mashtaka alieleza kuwa  wanawake hao hawakuruhusiwa kutoka ndani ya nyumba.  


Castro anakabiliwa na  mashtaka matatu ya utekaji nyara na ubakaji wa Amanda Berry, Gina De Jesus na Michelle Knight.  http://www.voaswahili.com
Previous
Next Post »