ADAM NDITI ASEMA YEYE SIO HATER, BUT ASEMA NI KWELI SHOW YA DIAMOND ILIKUA MBAYA
Mchezaji wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza, Adam Nditi amesema watu wasimwone kama ni hater baada ya kukosoa show ya Diamond nchini humo.
Kupitia Twitter, jana Adam alisema show ya Diamond ilikuwa mbovu nay a kutia aibu.
“Kwa wale wanaoniita hater kwa sababu ya tweet zangu kuhusu shoo ya Diamond juzi mimi namkubali sana Diamond na ni mshabiki wake mkubwa,” ametweet.
“Nazipenda nyimbo zake zote nazisikiliza karubuni kila siku ila juzi nilikuwa disappointed kwa sababu nilikuwa na matumaini makubwa ya shoo, ila ilikuwa haiko kwenye standard ambayo nilitegemea mmoja wa wasanii wakubwa wa Bongo kufanya.”
“Sasa jamani nadhani tunaelewana ukiniona hater endelea kuniita hater kama kuna kitu sikipendi ntasema sinyamazi,” amesisitiza mchezaji huyo mtanzania aliyechukua uraia wa Uingereza.
EmoticonEmoticon